October 8, 2020


 KESHO Oktoba 9 Klabu ya Yanga inayonolewa na Kaimu Kocha, Juma Mwambusi inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Mwadui FC.


Mchezo huo wa kirafiki utachezwa majira ya saa 1:00 usiku Uwanja wa Azam Complex.


Kiingilio kwa mzunguko itakuwa ni shilingi 3,000,(buku tatu) na VIP itakuwa ni 5,000, (buku tano).


Hivyo kwa wale watakaotoa buku tatu na buku tano kesho ni ruksa kuona udambwiudambwi wa Carlos Carinhos, raia wa Angola na Lamine Moro beki kisiki raia wa Ghana wakiendeleza pacha yao matata yenye mabao mawili ndani ya Ligi Kuu Bara.


Pia Fard Mussa mzawa naye ameshaanza kurejea kwenye ubora wake bila kuwasahau wengine akina Ramadhan Kabwili, Deus Kaseke pamoja na Juma Mahadhi.

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic