SALUM Kimenya, kiraka wa timu ya Tanzania Prisons amesema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri jambo analomshukuru Mungu.
Kimenya anasumbuliwa na nyama za misuli jambo ambalo limemfanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu na alikosekana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya JKT Tanzania uliochezwa Uwanja wa Jamhuri Dodoma kwenye sare ya kufungana bao 1-1. Oktoba 19.
Akizungumza na Saleh Jembe, Kimenya amesema kuwa hali yake inazidi kutengamaa kila siku kwa kuwa yupo kwenye uangalizi mzuri.
"Kwa sasa ninaendelea vizuri baada ya kuwa ninasumbuliwa na maumivu, kikubwa ninachomshukuru Mungu ni kwamba kila siku maendeleo yangu yanazidi kuimarika.
"Kikubwa ni kuona kwamba kila siku nakuwa imara na kufuata kanuni, mashabiki wasiwe na mashaka kuhusu mimi nitarejea uwanjani," amesema.
Kesho, Tanzania Prisons itakuwa na kazi ya kumenyana na Simba. Mchezo huo wa ligi utachezwa Uwanja wa Nelson Mandela.
0 COMMENTS:
Post a Comment