October 21, 2020


PATRICK Rweyemamu, Meneja wa Klabu ya Simba amesema kuwa kikosi kipo tayari kwa ajili mchezo wa kesho dhidi ya Tanzania Prisons utakaochezwa Uwanja wa Nelson Mandela.


Simba kwa sasa imeshatia kambi Rukwa ikiwa tayari kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa saa 10:00, Rukwa.


Inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushindwa kusepa na pointi tatu mbele ya Tanzania Prisons msimu uliopita wa 2019/20 na ilikwama kuifunga pia timu hiyo wakati huo.


Mechi ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Uhuru, Simba ililazimisha sare ya bila kufungana na ilipowafuata Uwanja wa Sokoine mchezo ulikamilika kwa sare ya bila kufungana.


Rweyemamu amesema:"Maandalizi yetu ni kwa mechi zote sio moja. Kila baada ya kumaliza mchezo maandalizi huwa yanakuwa kwa ajili ya mechi zijazo na ambacho kinatafutwa ni ushindi.


"Tupo tayari kwa ajili ya ushindani na tunaamini kwamba mchezo utakuwa mgumu lakini tunahitaji pointi tatu muhimu ili kuendelea kuyafuata malengo yetu tuliyojiwekea ya kutwaa ubingwa," amesema.


Simba ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi tano na Tanzania Prisons ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi sita baada ya kucheza mechi sita za ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic