October 21, 2020

 




BAADA ya Klabu ya KMC kugawana pointi mojamoja na Klabu ya Ruvu Shooting, jana Oktoba 20 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Uhuru kwa kufungana bao 1-1 akili zote za timu hiyo ni kuelekea mchezo wao ujao dhidi ya Yanga.

 Kwenye mchezo wa jana, KMC ilianza kupachika bao la kuongoza dakika ya 26 kupitia kwa Andrew Vincent lilisawazishwa na Shaban Msala wa Ruvu Shooting dakika ya 56.

Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa kukwama kwao kupata pointi tatu kwenye mchezo huo ni pigo kwao kwa kuwa walikuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani licha ya kuwa wageni kwenye mchezo huo.


"Tumeshindwa kupata ushindi ambao tulikua tunautarajia licha ya kuweza kuongoza kipindi cha kwanza. Haina maana kwamba tutaendelea kupata matokeo mabaya hapana tunajipanga kwa aili ya mechi zijazo.

"Wachezaji wametimiza majukumu yao na mashabiki pia ambao walijitokeza walituongezea nguvu ila mwisho wa siku tumeambulia pointi moja.Tunaanza maandalizi kwa ajili ya mechi nyingine, hiyo tumekwisha maliza," amesema.

Mchezo wa KMC dhidi ya Yanga utachezwa Oktoba 25, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.

KMC ipo nafasi ya saba na pointi zake kibindoni ni 11 baada ya kucheza mechi saba ndani ya msimu wa 2020/21, inakutana na Yanga ambayo ipo nafasi ya tatu na pointi 13 baada ya kucheza mechi tano.


9 COMMENTS:

  1. Lipuli walikuwa wanaikamia Yanga sasa wako FDL; Stand Utd walikuwa wanaikamia Yanga sasa wako FDL na nyie endeleeni kutafuta umaarufu kuikamia Yanga tu mtakipata mnachokitafuta

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bila shaka wanatafuta pointi 3 na Inshaallah watazipata

      Delete
  2. Safi sana KMC pigeni hao Utopolo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kama Simba walivyopigwa na Tanzania prison leo

      Delete
  3. Utopolo wao wanawaza tarehe Saba wslivyo na akili mbovu, ubingwa wsusahau kabisa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bila kubebwa na tff Simba hakuna kitu kabisa na bado

      Delete
  4. Wapi mzee wa billion 20 naona karibu atasusa timu huyo maana huwa hakawiagi huyo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic