October 31, 2020


JAMHURI Khwelo aliyewahi kuwa kocha wa timu hiyo amesema kuwa kikosi cha Simba kina matatizo makubwa mawili ambayo yanakisumbua kwa sasa jambo ambalo linawafanya wapate matokeo mabovu ndani ya uwanja.

Mabingwa hao watetezi wamekutana na vipigo viwili mfululizo na kuziacha alama sita zikisepa na upepo ndani ya Ligi Kuu Bara.

Walipoteza mbele ya Tanzania Prisons kwa kufungwa bao 1-0 wakiwa ugenini kwenye Uwanja wa Nelson Mandela kisha wakiwa nyumbani walitembezewa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Uhuru.

Leo Oktoba 31 Simba ina kibarua cha kusaka pointi tatu muhimu mbele ya Mwadui FC Uwanja wa Uhuru.

Julio amesema:"Kwa sasa Simba wanapambana na matokeo magumu kutokana na mambo mawili ambayo wanayo kwanza ni umri wa wachezaji wengi kuwatupa mkono jambo linalowafanya wapate tabu kuhimili mikikimiki ndani ya uwanja.

"Pili ni suala la majeruhi wengi ambao wapo kwa Simba kwa sasa, jambo hilo linafanya kocha awe kwenye wakati mgumu kutafuta matokeo na kuwa na kikosi kitakachoipa ushindi ndani ya uwanja.

"Wachezaji wakipata majeraha inachukua muda mrefu kupona na inapotokea ishu ya kubadilisha kikosi wengi wanashangaa na matokeo yanapokuja tofauti inakuwa ni makelele kwa mashabiki kwa kuwa hawajazoea kuona mambo hayo," amesema.


13 COMMENTS:

  1. Kumbe ni kweli mmesajili wazeee aahaaaaaa poleni sanaaa si mlisema hakuna kama nyie

    ReplyDelete
  2. Kweli umri ndio tatizo, vibabu vingi mno

    ReplyDelete
  3. Walisema tuwaache na wazee wao; leo wanalia na wastaafu wao.

    ReplyDelete
  4. hv mwandishi unamuliza julio jambo la kiufundi simba we unadhani kwa chuki yake ataongea nini!

    ReplyDelete
  5. Mzee anafungaje goli. saleh jembe usitafute kick kwa yanga

    ReplyDelete
  6. Julio bhana tangu msimu ulioisha Simba wamesajli wazee ajabu ndo mabingwa wa ligi mbele ya timu za vijana
    na mwambieni aweke kumbukumb tena ya hizi kauli zake baada ya gem kadhaa muende kumuuliza tena

    ReplyDelete
  7. Majeruhi sawa umri sio,kikosi kilchofungwa Na prison nani alizidi miaka 30?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Usijifanye hujui onyango na bocco wanamiaka mingap

      Delete
  8. Huyu sio kocha simba balii ni kocha aliyewahinkufundisha Simna na timu yake ya mwisho ni Dodoma mji aliyoshindwa kuipandisha daraja kwa kifupi ni kocha asiye na mafanikio kick zake anafikiri atazipata simba kwa kusaidiwa na mwandishi mwenye kadi ya uanachama yanga

    ReplyDelete
  9. Simba ile yakina mkude na Ndemla Julio alisikika akisema tatizo la simba imesajili wavulana ndio kitu kilichokuwa kinawasumbua.Leo kuona julio anasema hivi kwa kweli inashangaza sana, Yaani Julio angekuwa mbunge angesutwa kila siku bungeni. Ame nae ni mzee,Miraji Athumani ni majeruhi nae ni mzee,simba kuna Ali salim .mbadala wa manula au kakolanya ,Kennedy juma na Ame badala ya wawa au Joshi ,David kameta mbadala wa kapombe,kuna kamagu mbadala wa shabalala,kuna Ndemla,
    ajibu,Muzamiru,Charles ilanfya,miraji hao wote ni wazawa na vijana wenye umri wa kucheza mpira kwenye mazingira yeyote yale ya ujana.yaani simba kama kuna timu imesjili kitaalam kwenye ligi kuu bara basi ni simba kwani wana timu nzima ya vijana ndani ya timu.Na raha zaidi hawa vijana wengi wao ni wazawa. Maana yake nini? Kama simba watamuajiri mwanasaikolojia mahiri wa kukaa na hawa vijana na kuwapika kiakili wakapikika mwakani simba hana haja ya kusajili mchezaji wa nje hata wa ndani.Nampa challenge Mo najau yupo smart na anawashauri mahiri ila kuna kitu wanakosea nacho ni kuacha vipaji hivi vilivyomo ndani ya simba vikipotea kila mwaka. Kumbuka simba hawasjili mchezaji mbovu wa ndani.Mchezaji anakuwa mbovu akija simba hasa wazawa. Tatizo nini? Tatizo hawa vijana wanakosa professional psychologist mahiri wa kuzieka au kuzitengeneza akili zao zikawa imara zaidi kwenye mazingira mapya kuliko huko walikotoka maana walichokitarajia sio kukaa benchi hapa simba malengo yao kuwa mastaa zaidi. Kitendo cha kukaa benchi huwa kinawachanganya akili na kukata tamaa,huwatoa mchezoni wachezaji vijana.Hata ukimsikiliza saimoni msuva atakwambia mtaalamu wa akili ndie aliembakisha mchezoni na kudumu kwenye kiwango chake hadi leo.Kwa wenzetu Dataktari wa akili kwenye timu ni muhimu kuliko kocha mkuu. Ila sharti lake ni lazima daktari wa akili awe well qualified kwenye taaluma yake la sivyo badala ya kuwajenga akili wachezaji atakuwa anawachanganya akili it is very sensitive kind work.

    ReplyDelete
  10. Uzuri wa Julio huwa hafichi maradhi mnataka afiche kuwa mmesaji wazee? msemakweli mpenzi wa mungu sipati picha mkianza kimataifa na hao wazee

    ReplyDelete
  11. Kwa Simba hii mwaka huu tutashuhudia makapu ya magori kimataifa sababu wazee pumzi imekata mapemaaaa

    ReplyDelete
  12. Azam nao wamesajili wazee maana gari linzanza kukata upepo.kuna watu wana mongwa zao na simba wamekaa wakisubir nakuomba timu ifanye vibaya wapanue midomo yao. Timu gani isiofungwa Duniani yaani mambo mengine ushuzi mtupu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic