LIGI ya Mabingwa Barani Afrika imeendelea mwishoni mwa wiki hii, ikiwa ni hatua ya nusu fainali kwa miamba ya soka Afrika ya Kaskazini Morocco na Misri kutoana jasho vilivyo, ambapo National Al Ahly wakiwa chini ya kocha mpya Pitso Mosimane walikuwa ugenini kuvaana na Wydad Casablanca ya Morocco.
Kwenye mchezo huo Al Ahly iliweza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 na kujiweka katika mazingira mazuri katika mechi ya marudiano itakayochezwa Misri.
Pitso Mosimane ambaye ajiuzulu kuifundisha Mamelodi Sundowns ya Afrika ya Kusini mara baada ya kutwaa ubingwa, ameonyesha ni kwa jinsi gani anaweza kuipa taji Al Ahly la Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi huo wa ugenini wakisubiri kumaliza kazi nchini Misri.
Timu hiyo ambayo inaongoza kwa utajiri Afrika ilifunga magoli yake kupitia kwa Mohamed Magdy dakika ya nne na bao la pili likiwekwa kimiani na Ali Maaloul kwa mkwaji wa penati dakika ya 62.
Nusu fainali nyingine iliwashuhudia Raja Casablanca wakiwakaribisha vigogo wengine, Zamelek wa Misri ambapo walikubali kipigo cha bao 1-0 bao pekee la Zamelek likifugwa na Achraf Bencharki dakika 18 ambapo mechi za marudiano zitachezwa tarehe 23 mwezi huu.
Huenda ikashuhudiwa fainali kati ya timu za Misri ila ni jambo la kusubiri baada ya wiki moja majibu yatapatikana.
0 COMMENTS:
Post a Comment