BAADA ya jana, Oktoba 18 Zubeir Katwila aliyekuwa Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar kubwaga manyanga na kuibukia ndani ya Ihefu FC akiwa ni Kocha Mkuu, Uongozi wa Mtibwa Sugar umemshukuru kwa kutumika ndani ya timu hiyo.
Katwila amelelewa Mtibwa Sugar ambapo alianza akiwa ni mchezaji wa timu hiyo 1999 na jana Oktoba 18 alihitimisha safari yake ya mafanikio na timu hiyo kwa kuibukia ndani ya Ihefu.
Uongozi wa Mtibwa Sugar kupitia kwa Ofisa Habari, Thobias Kifaru umesema :"Ahsante kwa kumbukumbu ulikuwa na wakati mzuri hapa na hapa ni nyumbani.
"Wewe ni kijana wetu na umekuwa ndani ya Mtibwa kwa mafanikio makubwa, bado ni ndugu yetu na kila la kheri kwenye maisha mapya,".
Leo Mtibwa Sugar itakuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Namungo FC Uwanja wa Jamhuri na Katwila ataanza kazi kesho ambapo Ihefu itamenyana na Azam FC, Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
0 COMMENTS:
Post a Comment