BAADA ya kupiga asisti za kutosha, kiungo mshambuliaji wa Simba raia wa Msumbiji, Luis Miquissone amesema kuwa hivi sasa akili na nguvu anazihamishia kwenye kufunga mabao.
Kiungo huyo ndiye anayeongoza hivi sasa katika asisti ambaye amepiga tano pekee hadi hivi sasa huku akifunga bao moja pekee kwenye mchezo uliopita wa Ligi Kuu Bara walipocheza na JKT Tanzania.
Luis amesema kuwa majukumu yake katika timu siyo kupiga asisti pekee, lingine ni kufunga mabao yatakayowawezesha kupata ushindi.
Luis amesema kuwa ndani ya wakati mmoja amejipanga kupiga asisti na kufunga mabao baada ya kufunga moja katika mchezo dhidi ya JKT.
Aliongeza kuwa amepanga kuanza na hilo la kutumia vema kila nafasi atakayoipata kwa kufunga mabao katika michezo ijayo ya ligi ukiwemo unaofuatia dhidi ya Tanzania Prisons kwenye Uwanja wa Nelson Mandela huko Sumbawanga utakaopigwa Oktoba 22, mwaka huu.
“Kutengeneza nafasi za kufunga mabao ni moja ya majukumu yangu niliyopewa na kocha wangu kwa kunitaka kuwatengenezea wenzangu kwa faida ya timu.
“Kufunga pia ni moja ya jukumu nililopewa na kocha ambalo nimepanga kulifanyia kazi katika michezo ijayo kwa kuhakikisha ninatumia vema kila nafasi nitakayoipata ya kufunga baada ya kufunga bao moja pekee mechi dhidi ya JKT Tanzania.
“Kwani ninapotoka uwanjani bila ya kufunga sijisikii vizuri licha ya kupiga asisti, hivyo ndani ya wakati mmoja nitahakikisha ninatengeneza asisti na kufunga mabao zaidi kwa kuanzia mchezo ujao wa ligi tutakapocheza na Prisons,” alisema Luis.
michezo mingi mbeleni.
“Bado kuna michezo mingi sana huko mbeleni ya ligi kuu ambayo naamini nitakuja kucheza, kwa sasa bado ni mapema sana kwani hata robo ya msimu hatujaufikia hivyo natarajia kupata nafasi ya kucheza,” alisema mshambuliaji huyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment