October 18, 2020


 PRINCE Dube, nyota wa Klabu ya Azam FC ameonekana kuutikisa ufalme wa Meddie Kagere wa Simba baada ya kuhusika kwenye mabao nane ndani ya timu yake kati ya 12 huku Kagere akihusika kwenye mabao manne kati ya 14 kwa msimu wa 2020/21.

Dube, raia wa Zimbabwe alianza kwa makeke mchezo wake wa kwanza dhidi ya Polisi Tanzania alipotengeneza pasi yake ya kwanza kwa Obrey Chirwa na aliweza kufunga mabao mawili mbele ya Coastal Union na timu yake ilisepa na pointi sita mazima kwenye mechi mbili za mwanzo zilizochezwa Uwanja wa Azam Complex.



Aliweza kuwa sehemu ya kikosi wakati Azam FC ikishinda ba 1-0 dhidi ya Mbeya City na aliibukia Uwanja wa Nelson Mandela kwa kufunga bao lake la tatu wakati timu yake ikishinda bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.


Kwa mwezi Septemba aliweza kufunga mabao matatu na kutoa pasi moja ya bao wakati timu yake ilipokusanya pointi 12 na kuwa nafasi ya kwanza na alitwaa tuzo ya mchezaji bora kwa mwezi huo pamoja na Kocha Mkuu Arstica Cioaba wa Azam FC.


  Mabao mawili alifunga kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Azam FC iliposhinda mabao 4-2 na alitoa pasi ya bao kwa Chirwa.


Pia alifunga kwenye mchezo mwingine dhidi ya Mwadui FC wakati Azam FC ikishinda kwa mabao 3-0 na kumfanya afikishe jumla ya mabao sita kibindoni akiwa ni kinara kwenye mbio za ufungaji.

Jumla amehusika kwenye mabao nane kati ya 12 akimpoteza Kagere wa Simba ambaye amehusika kwenye mabao manne kati ya 14 aliyafunga mbele Biashara United, Gwambina na JKT Tanzania ambapo aliwafunga mabao mawili.

Vita yao imeanza kupamba moto ambapo Dube ni kinara kwa kutupia akimpoteza Kagere ambaye ana tuzo ya mfungaji bora aliyoitwaa msimu uliopita baada ya kufunga mabao 22.

 

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic