UONGOZI wa Simba umesema kuwa mchezo wa leo dhidi ya Mlandege FC utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex saa 11:00 jioni ni maalumu kwa ajili ya kukiweka sawa kikosi hicho.
Simba ni mabingwa watetezi wana kibarua cha kuufunga mwezi Oktoba kwa kucheza na Tanzania Prisons, Oktoba 22, Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.
Simba inanolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji akisaidiana na mzawa, Seleman Matola wameongoza mechi tano za ligi na kushinda nne huku wakiambulia sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Leo benchi la ufundi litakuwa na kazi ya kukiongoza kikosi hicho kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege FC kutoka Visiwani Zanzibar.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanatambua wana kazi ngumu ya kucheza na Prisons ila kabla ya kukutana nao watacheza mechi ya kirafiki kujiweka sawa.
"Tuna mechi ngumu za kucheza ila tupo tayari na kabla ya kukutana na wapinzani wetu Tanzania Prisons tutaanza kutoa burudani leo mbele ya Mlandege kwenye mchezo wa kirafiki utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex.
"Mashabiki wetu ni wakati wa kujitokeza kwa wingi uwanjani kushuhudia burudani ambayo ilikuwa imekosekana kwa muda mrefu," amesema.
Simba nguvu moja twende zetu chamazi tukaisapoti timu yetu? This is simba another level
ReplyDeleteI love Simba Sports Club
ReplyDeleteMikia fc mnahamasishana unyumbu tu
ReplyDelete