KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck akisaidina na Kocha Msaidizi Seleman Matola baada ya kuwasili Mbeya leo Oktoba 19 kimefanya mazoezi kwa ajili ya kurejesha miili ya wachezaji kwenye ubora wao.
Oktoba 17 kilikuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Mlandege FC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na kiliibuka na ushindi wa mabao 3-1.
Mazoezi hayo ambayo ni maandalizi kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons yamefanyika Uwana wa Sokoine, Mbeya.
Simba itamenyana na Tanzania Prisons, Oktoba 22, Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa saa 10:00 jioni.
Tanzania Prisons ambao ni wenyeji wa mchezo huo leo walikuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya JKT Tanzania, mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.
Mchezo huo umekamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na kuzifanya timu hizo kugawana pointi mojamoja leo Oktoba 19.
0 COMMENTS:
Post a Comment