October 19, 2020

 


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze leo Oktoba 19 kimeendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Polisi Tanzania kwenye kambi yao iliyopo maeneo ya Kigamboni. 


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Oktoba 22, Uwanja wa Mkapa saa 1:00 usiku unatarajiwa kuwa na ushindani kwa timu zote mbili kuwania pointi tatu muhimu.

Msimu uliopita wakati wakisaka pointi sita kwenye mechi mbili za Ligi Kuu Bara, Yanga iliambulia pointi mbili sawa na Polisi Tanzania walipokutana uwanjani.


Mchezo wa kwanza, Uwanja wa Uhuru ngoma ilikuwa ni sare ya kufungana mabao 3-3  na ule wa pili Uwanja wa Ushirika, Moshi ngoma ilikuwa 1-1 msimu wa 2019/20.


Mechi ya mwisho kwa Yanga ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania, leo Oktoba 19 imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Gwambina FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic