KIKOSI cha Yanga leo Oktoba 6 kimerejea kambini rasmi kwa ajili ya kujiandaa na mechi zake zinazofuata za Ligi Kuu Bara ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Simba itakayopigwa Oktoba 18.
Baada ya Oktoba 3 kutangaza rasmi kuachana na aliyekuwa Kocha Mkuu, Zlatko Krmpotic raia wa Serbia kwa kile walichoeleza kutokubali falsafa yake kikosi kipo chini ya Juma Mwambusi.
Mchezo huo wa mwisho kwa Krmpotic alishinda mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union, Uwanja wa Mkapa. Na unaingia kwenye rekodi za mchezo ambao aliongoza kikosi chake kufunga mabao mengi ndani ya dakika 90 kwa kuwa mechi zake nne za ligi alikuwa anafunga bao mojamoja.
Mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Simba, Oktoba 18, Uwanja wa Mkapa na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu zote kufanya usajili mzuri na wachezaji kuwa na maelewano mazuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment