October 6, 2020

 


UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa sasa umewapa mapumziko wachezaji wake ambao hawajaitwa timu zao za taifa kwa muda wa siku mbili kabla ya kurejea kambini kuanza maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara.

Mchezo wao wa mwisho raundi ya tano, Simba ilishinda mabao 4-0 dhidi ya JKT Tanzania kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Akizungumza na Saleh Jemb, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa kwa sasa wachezaji wapo mapumziko huku wengine wakiwa kwenye kambi za timu zao za taifa.

"Kwa sasa wachezaji wapo kwenye kambi zao za taifa kwa na wale ambao hawapo kambini hawajaitwa kwenye timu zao za taifa wamepewa mapumziko kwa muda wa siku mbili.

"Kila kitu kipo sawa na tuna amini kwamba kila mchezaji anatimiza majukumu yake huko alipo, imani yetu ni kuendelea kufanya vizuri kwenye mechi zetu zote," amesema.

Miongoni mwa wachezaji walioitwa timu zao za taifa ni pamoja Clatous Chama wa Zambia, Luis Miquissone wa Msumbiji huku wazawa ikiwa ni pamoja na Said Ndemla, Jonas Mkude na John Bocco.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic