IMEBAKI siku moja kuanzia sasa kabla ya kuchezwa ile mechi ya watani wa jadi ambayo inasubiriwa kwa shauku na wadau ndani ya Bongo ile ya Yanga na Simba.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Novemba 7 Uwanja
wa Mkapa na tayari kwa sasa viingilio vimewekwa wazi hivyo kila mmoja yupo na
chaguo lake akijua kwamba wapi atakwenda kukaa.
Mbali na kutambua viingilio pia maandalizi kwa
timu zote naona yanaendelea kwa kuwa ili timu iingie uwanjani ni lazima
ijipange kufanya kweli kabla ya mechi.
Kikubwa ambacho kinatakiwa ni mashabiki,
wachezaji kuamini kwamba hakuna timu yenye uhakika wa kushinda kila timu ina
nafasi ya kushinda ikiwa itafanya maandalizi mazuri.
Masuala ya kuingia na matokeo uwanjani muda wake
umekwisha dakika 90 zitaamua nani ni nani na kwa nini apate matokeo hayo.
Atakayeshinda atajulikana baada ya dakika 90 ikiwa ni mwenyeji Yanga sawa ama Simba mgeni sawa hata sare pia inawezekana kikubwa ni kwa timu zote kufanya maandalizi mazuri.
Waamuzi ambao watapewa kazi ya kuchezesha mchezo
huu wana jukumu la kuwa makini katika kutimiza sheria 17 kwa kuwa kwa mechi za
hivi karibuni wengi wamekuwa wakivurunda.
Sehemu ya kona iwe kona, sehemu ya faulo ipigwe
tu hakuna tatizo na penalti pia zitolewe zile halali na sio ilimradi penalti,
kikubwa ni umakini ili kuepuka lawama.
Nina uhakika Shirikisho la Soka Tanzania(TFF)
litakuwa na umakini katika hili kwa kusimamia kila kitu kiende sawa na isiishie
kwenye mechi za Yanga na Simba pekee hapana lazima iwe kwenye mechi zote za
ligi.
Kila mchezo ambao unachezwa uwanjani unahitaji
kutazamwa kwa umakini na waamuzi nao wana jukumu la kufuata sheria 17 za mpira
ndani ya uwanja.
Kuna kasumba yakuzitazama kwa ukaribu hizi mechi
za dabi jambo ambalo linadumaza soka letu. Muhimu kwa kila timu kupewa
kipaumbele na kuona kwamba kila timu ni sawa ndani ya uwanja.
Kwa upande mwingine sasa tayari ligi kuu imezidi
kushika kasi kwa kuonyesha ushindani mkubwa.Rai yangu kwa timu zote kuhakikisha
kwamba zinapambana na kufanya maandalizi mapema.
Tumeona kwenye upande wa usajili wapo ambao
wamefanya vizuri na wengine wamebuma kikubwa ni timu katika hili ni kuwaandaa
pia watu wa scauti iliwaweze kuwatambua wachezaji ambao watawasaidia wakati wa
dirisha la usjili wasipate tabu kama wakati mwingine.
Maandalizi kwa kila timu yanapaswa kuwa mapema na
sio ya kukurupuka kwa kuwa matokeo yake huwa hayawi mazuri hata mara moja hivyo
muda ni sasa kwa kila timu kulitambua hilo.
Ushindani unaleta raha hasa kwa matokeo ambayo
yanapatikana inaonesha kabisa kwamba timu zote zimejipanga kiasi cha kutosha
hakuna mnyonge licha ya changamoto ambazo haziwezi kuzuilika.
Waamuzi yawapasa kuongeza umakini ndani ya uwanja
kwa kuwa tayari tumeanza kuona lawama ambazo znatokea mara kwa mara kwa ajili
yao hivyo ili kuzidisha utamu wa ligi yawapasa wawe nao makini pia.
Jambo lingine ni kuhusu Ligi Daraja la Kwanza
ambayo imekuwa ikiwekwa nyumanyuma kama mfuko wa koti hasa katika uangalizi
wake na usimamizi wake.
Kwa kweli mazingira ambayo wanayapitia sio rafiki
kwa kuwa kuanzia miundombinu mpaka vifaa vyote ni vya chini zaidi hivyo
kuwafanya wengi kuandelea kushiriki mashindano haya kwa kuungaunga jambo ambalo
linaua uwezo wa timu zetu.
Timu ili iwe bora ni lazima ipate maandalizi
mazuri hata ligi ambayo inashiriki pia yapaswa kuwa na ushindani hali ambayo
itasaidia kuweza kupata mshindi wa kweli hapo baadaye mara baada ya kupanda
daraja.
Timu ambazo zinashiriki Ligi Daraja la Kwanza
ndizo ambazo zikipata nafasi zinashiriki ligi kuu hivyo zinapaswa nazo pia ziwe
na waangalizi ambao watazisaidia katika kupambana ili zikipanda daraja ziweze
kuwa na ushindani ule ule na sio kuanza kuyumba.
Katika kufanikisha hilo ni wajibu wa bodi ya ligi
kuandaa mazingira kwa ajili ya timu ambazo zinashiriki Ligi Daraja la Kwanza
kuweza kuwa na mdhamini ambaye atasaidia kuongeza ushindani.
Kwa kufanya hivyo kutaongeza hamasa za timu
shiriki kuweza kujiandaa mapema hata kabla hazijapanda kwa kuwa kutakuwa na
ushindani wa kweli katika kila hatua ambayo wanapitia na kuweza kufanya kusiwe
na tofauti kubwa muda watakaopanda daraja.
Pia itarahisisha kwa timu kuweza kuwa na
mahusiano mazuri na kampuni mbalimbali hali itakayosaidia kuweza kupata
wadhamini kutoka sehemu tofautitofauti hata pale ambapo watapanda daraja kutoka
pale ambapo walikuwa awali kiushindani.
Kila kitu kikiwa kwenye mpangilio imani yangu ni
kwamba ule muda wa kuwa wasindikizaji utakuwa umekwisha na badala yake tutakuwa
na vipaji ambavyo vitasaidia kukuza vipaji wa timu zetu pamoja na ushindani.
Kitu cha kuzingatia ni kuhakikisha kwamba kila
mmoja anatimiza jukumu lake kwa wakati bila kutegeana na kukumbushana kwamba
maendeleo ya mpira hayaji ghafla bila kutarajiwa ni lazima kuwe na mikakati
imara ambayo itasaidia kuwa na sera ambazo zitazaa matunda.
Hakuna mafanikio ambayo hutokea kwa bahati mbaya
bali ni kupitia kujituma na kuhakikisha kwamba vile vipaji ambavyo vinakuzwa na
kulindwa na sio kupotea bila kuwa na malengo yoyote itatufanya tuzidi kuwa
wasindikizaji kila siku.
Apigwe 5 kandambili aka vyura aka GONGOWAZI tuufunge mwaka inshaallah
ReplyDeleteKuma we , 5 atapigwa mama yako, nguruwe fc wewe
ReplyDeleteAcha matusi wewe tushakupiga tano Mara ngapi mpaka sasa. Tunakupiga tena Kama Kama kawaida yetu kuwachapa tano.
DeleteAchen matusi toeni hisia zenu sio matusi bado mwamuzi atakuwa dk 90
ReplyDeleteYanga wamekuja wakati mbaya sana, yaani watapigwa manyani hawa hadi watamkumbuka Luc Eymael, maana walau alishaanza kuwajengea wachezaji uelewano. Huyu Mrundi amekuja ni kama anaheshimiwa tu, ila bado timu haieleweki vile, kichaka kilichopo ni kauli kwamba 'kocha apewe muda'
ReplyDeleteSasa matusi ya nini nyie wadau, badilikeni acheni ushabiki wa kishamba huo. Matusi hayana nafasi ktk mpira, cc ni watani Wa jadi na si mahasimu, naomba tuelewane.
ReplyDeletesasa hapo mshindi yuko wapi, kilaza ww
ReplyDelete