INAELEZWA kuwa Kelvin Yondani beki wa zamani wa Klabu ya Yanga yupo kwenye hesabu za kuibukia ndani ya Coastal Union ya Tanga.
Beki huyo mwenye uwezo mkubwa ndani ya uwanja aliachana na Klabu ya Yanga msimu uliopita baada ya kushindwana kwenye suala la maslahi.
Yondani pamoja na Juma Abdul walikuwa kwenye mazungumzo na Yanga kabla ya kushindwa na uongozi wa Yanga kuwatakia kila la kheri kwenye maisha yao mapya.
Nyota huyo alikuwa anatajwa kuingia ndani ya anga za Namungo ambao waliweka wazi kwamba wanamheshimu mchezaji huyo ila hawajampa mkataba.
Kwa sasa Coastal Union inapambana kuboresha kikosi hicho ambacho kiliondokewa na nyota wao wawili kwenye safu ya ulinzi wakiongozwa na Bakari Mwamnyeto ambaye yupo Yanga na Ibrahim Ame ambaye yupo zake Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment