KIUNGO wa Simba, Bernard Morrison ameachwa kwenye msafara wa wachezaji uliokwea pipa leo Desemba 18 kuwafuata wapinzani wao FC Platinum ya Zimbabwe.
Nyota huyo ambaye alisajiliwa kwa mbwembwe akitokea Klabu ya Yanga kwa dili la miaka miwili amekuwa hana nafasi ndani ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck.
Mbali na Morrison nyota mwingine ambaye ameachwa ni Charles Ilanfya ambaye sio chaguo la Sven licha ya uongozi kuweka wazi kwamba usajili wa mchezaji huyo kutoka Klabu ya KMC ilikuwa ni pendekezo la kocha huyo.
Simba imewafuata FC Platinum ikiwa na orodha ya wachezaji 24 ambapo wanatarajiwa kucheza FC Platinum Desemba 23, mchezo wa kwanza kisha ule wa marudiano itakuwa ni kati ya Januari 5-6, Uwanja wa Mkapa.
Nafasi ya Morrison imechukuliwa na kiungo mpya Taddeo Lwanga ambaye ni ingizo jipya akiwa amesaini dili la miaka miwili.
Jamani, jamani mwandishi ndivyo walivyosema? Kwani wataenda wachezaji wote jamani?
ReplyDeleteMorrison ana matatizo gani ya kiafya hadi aachwe kwenye msafara?Uongozi utoe tamko ili tujue sababu za yeye kuachwa
ReplyDeleteMTAKA NYINGI NASABA!!!!!!!!
ReplyDeleteWaandishi wenzako wamefatilia mpaka wamejua ni mgonjwa ila nyinyi.mnakimbilia kuandika umbeya
ReplyDeleteMmmmh kumwacha bernd Morrison ni dalili ya kufungwa
ReplyDeleteMbinu za mpira, hii Ni silaha yakuja kuwamalizia kwamkapa.
ReplyDeleteBiashara asubuhi jioni mahesabu
DeleteNa bado
ReplyDeleteDUH
ReplyDelete