December 19, 2020

 


NYOTA wa Klabu ya Simba, Bernard Morrison amesema kuwa kwa sasa bado hajajua nini kinachomsumbua kwa kuwa hajapewa majibu baada ya kulazwa kwenye hospitali iliyopo Dar akipatiwa huduma.


Nyota huyo hayupo kwenye kikosi cha wachezaji 24 waliokwea pipa jana na kuibukia Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.


Simba ilitua salama nchini Zimbabwe na imeanza maandalizi mapema kwa ajili ya mchezo huo wa kwanza unaotarajiwa kuchezwa Desemba 23.

Kwenye Ligi Kuu Bara, Simba ikiwa imecheza jumla ya mechi 14 na kufunga mabao 33 yeye amefunga bao moja na kutoa pasi moja ya bao.

Morrison amesema:"Nipo hospitali kwa sasa nilikuwa ninajskia vibaya nikaamua kupata vipimo ili nipate matibabu, baada ya vipimo nitajua nini kinachonisumbua.

Hivyo chanzo cha nyota huyo kuachwa kwenye msafara huo ni kutokana na kutokuwa sawa kiafya jambo ambalo limemfanya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck amuache.


Mbali na Morrison nyota mwingine ambaye yupo Bongo ni mshambuliaji, Charles Ilanfya ambaye hajawa kwenye mpango wa Sven.

Chanzo:Championi

6 COMMENTS:

  1. sasa mbona juzi mliandika eti ameachwa kwa sababu ya utovu wa nidhamu..akiwa Yanga mbona aliachwa mara nyingi tu wakati timu ikisafiri mikoani , na hata akiwa Dar kuna kipindi yeye na Yondani walikuwa hawahudhurii mazoezi..Anawakera ndiyo maana hamwezi maliza siku bila kumuandika..Yeye na saio wenu

    ReplyDelete
  2. Kwa kiasi kikubwa sana nawalaumu simba na wale wapenzi wa simba wanaojifanya simba lialia lakini wanashindwa kupambana kwenye masuala ya msingi kwa timu yao. Yanga waliapa au kujiapiza kwa kusema kuwa Morrison hatocheza simba iwe kwa figisu ya aina yeyote ile kwa Ushirikina au siasa chafu za nje na ndani ya uwanja lakini watahakikisha Morrison hachezi simba. Sasa lao ninapoona Morrison anaandamwa kwa mambo ambayo kimsingi ni ya kawaida sana kiasi cha kumtoa mchezoni huwa nasikitika sana.Yaani wale wazee wa kamati ya roho mbaya ya simba wapo wapi? Au wamezidiwa gemu na Yanga? Ni kocha Sven aliejitoa fahamu na kumtetea Morrison bila ya uiga na nampongeza sana kocha Sven kwa ujasiri wake kwenye suala la Morrison.Kuna vitendo vingi tu vya aibu kutoka kwa wachezaji lakini haikuwa jambo kwenye timu zetu.Kuna wachezaji wamepiga wachezaji wenzao uwanjani,kuna wale waliowatemea mate wenzao usoni,kuna wale waliowapapasa wenzao sehemu za siri na kuna wale waliohusishwa na hongo lakini haikuwa jambo ila Morrison imekuwa kama vile watu wanasubiri ajikwae kidogo watu watengeneze story za kummaliza.si mtetei Morrison kutokana na matendo yake ambayo yapo kinyume na professional yake ila hakuna binaadamu mkamilifu na inaonekana anakamiwa mno kiasi kana kwamba watanzania tunataka kujiingiza kwenye zambi za ubaguzi.Morrison ni mchezaji mzuri mno na ndio maana Yanga hawatamami kuona Morrison akionesha uwezo wake kamili akiwa simba na wamefanikiwa kuwaaminisha watu kuwa Morrison ni mchezaji mtukutu ili wapate nafasi ya kusema tulikwambieni.Kama kweli Yanga wanaamini Morrison ni mchezaji mtukutu kwanini mpaka leo wamng'ang'anie kuwa bado ni mchezaji wao?Nitawashangaa sana na kiasi fulani nawashangaa sana simba kukubali kuingizwa kwenye siasa za sumu za watani wao jadi za kummaliza Morrison.

    ReplyDelete
  3. Good points,, wana simba tuamke ss, kamati ya roho mbaya ujumbe huo wa hapo juu ufuatiliwe kwa kina p/se!

    ReplyDelete
  4. Mwandishi una ukilaza fulani kwa sababu mwanzoni uliandika tuhuma bila kuthibitisha sasa ukweli umejulikana ni afadhali ungenyamaza

    ReplyDelete
  5. Morrison anasumbilwa na physiological disorder... Nusu wazimu.. Hawezi kucheza mpira Tanzania,arudi kwao... Angekuwa mzima asinge wa geuka Yanga.Useless player.

    ReplyDelete
  6. Kwa kiwango cha Morrison kama angekuwa Hana matatizo hata Yanga wasingweza kumsajili, kumbuka Yanga walimkuta Hana team kwa miezi kadhaa, inahitaji akili ya ziada kuelewa Kwann alikua hana team kama ni mchezaji mwenye Nidhamu?
    Time will tell tell, lkn kwa asilimia kubwa inaonekana hayupo sawa...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic