December 19, 2020

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umekamilisha kila kitu kuhusu usajili wa nyota wao Saido Ntobanzokiza, raia wa Burundi.

Kiungo huyo mshambuliaji amejiunga na timu hiyo akiwa ni mchezaji huru alikuwa anacheza timu ya taifa ya Burundi.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa kila kitu mchezaji huyo hivyo kuanza kwake leo kwenye mchezo wa Ligi uu Bara dhidi ya Dodoma Jiji ni kazi ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze.

"Tumekamilisha kupata  leseni na vibali vya mchezaji wetu Saido Ntibazonkiza hivyo kuanza mechi ya leo ni kazi ya benchi la ufundi.

"Maandalizi yapo vizuri na kila mchezaji anajua kwamba tunahitaji kupata pointi tatu hilo lipo wazi kwani mpaka sasa tunakwenda vizuri.

"Tunawaheshimu wapinzani wetu kwa kuwa ni timu nzuri ila wanakutana na timu ambayo ina wachezaji wazuri na wanahitaji pointi tatu," .

Baada ya kujiunga na Yanga kwenye dirisha dogo, nyota huyo amecheza mchezo mmoja wa kirafiki wakati Yanga ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Singida United.

Uwanja wa Liti ambao zamani ulikuwa unaitwa Namfua yeye alifunga mabao mawili na bao lingine lilifungwa na Deus Kaseke.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic