December 18, 2020


KLABU ya Yanga leo Desemba 18 imeongeza mkataba na kiungo mshambuliaji Haruna Niyonzima kutokana na Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze kukubali uwezo wake.

Nyota huyo raia wa Rwanda amekuwa kwenye uwezo mkubwa ndani ya kikosi hicho licha ya kukosa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.

Kiungo huyo ambaye anaushkaji pia na nyavu akiwa ametupia bao moja kati ya 22 ambalo alifunga mbele ya Coastal Union, Uwanja wa Mkapa ameongeza dili la mwaka mmoja. 

Niyonzoma alirejea kikosini baada ya kusepa na kuibukia nchini Rwanda ambapo alikwenda kujiunga na timu ya taifa ambayo ilikuwa inashiriki michuano ya Afcon.

Kwa mujibu wa Injinia Hersi Said ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu ya Yanga amesema kuwa Kaze ametoa ripoti ambayo itatumika kwenye usajili.

Ripoti hiyo imeelekeza wachezaji ambao watatolewa kwa mkopo na wale ambao wataongezwa ndani ya kikosi hicho ambacho kesho kitakuwa na mchezo wa ligi dhidi ya Dodoma Jiji, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

"Tupo vizuri kwa ajili ya kufanya usajili ambao ni pendekezo la mwalimu, ripoti ipo tayari na tutaitumia katika kuboresha kikosi ili kiwe bora.

"Wapo wachezaji ambao wataongeza mkataba ndani ya timu, wengine wataondolewa kwa mkopo pia wapo ambao wataongezwa ndani ya timu.

"Tayari tumekamilisha usajili wa kiungo mshambuliaji Saido Ntibanzokiza ambaye yeye kila kitu kimekamilika kilichobaki kwa sasa ni mwalimu mwenyewe kuamua kumtumia akiona inafaa," . 

4 COMMENTS:

  1. TUnasajili wazee halafu kazi yetu kuwatolea mimacho mikia.
    Hivi kweli Haruna na Saido ni wachezaji wa kuwasajili kama tunadai tunataka wachezaji wa baadaye.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mikia gani? Hao walionunua mechi

      Delete
    2. Kwenye wazee aliaribiki jambo tuna wazoefu (maestro) wa nchi mbili Rwanda na Burudi wakichanganyika na watoto kina Fei Yassa Kisinda Mwamyeto hilo linatoka bonge la mixed Grill la Ubingwaaaaaa@UnknownDecember 18, 2020 at 6:41 PM

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic