WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Klabu ya Simba, leo Desemba 18 wamewasili salama nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wa hataua ya kwanza dhidi ya FC Platinum.
Kikiwa chini ya Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck na kocha msaidizi Seleman Matola kimepata bahati ya kuonana na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe, Profesa Emmanuel Mbennah.
Balozi huyo alipata nafasi ya kupiga picha ya pamoja na viongozi, wachezaji na benchi la ufundi baada ya chakula cha mchana.
Pia amepata nafasi ya kuongea na wachezaji wa timu ya Simba ambao wana kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Kikiwa kimeongozana na wachezaji 24 wanaoongozwa na nahodha John Bocco pamoja na Mohamed Hussein, 'Tshabalala' atakosekana mpanda mpira Bernard Morrison na Charlse Ilanfya ambao hawapo kwenye mpango wa Sven.
mpanda mpira hata alivyokuwa na Yanga alikuwa anabaki sana Dar....kwa sababu ya kucheleweshewa mshahara..isiwe gumzo.tujadili milion 600 za Morrison zitaingia lini Yanga
ReplyDeleteKweli ikuambiwa akili zako kama mshabiki wa yanga pigana , alafu cha ajabu akili zao kama zinafanana kuanzia vinogozi wao hadi washabiki wao teh teh teh teh tehn teh
ReplyDelete