December 18, 2020


 JUMLA ya mabao 9 yamekusanywa leo Desemba 18 kwenye mechi tatu za mwanzo ndani Ligi Kuu Bara. 


Mchezo mmoja umekamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1 huku mechi mbili timu mbili zikisepa na pointi tatu na mabao matatu.


Ilikuwa namna hii:-


Mwadui 1-1 Polisi Tanzania, Uwanja wa Mwadui Complex. Polisi Tanzania walianza kupata bao la kuongoza dakika ya 17 kupitia kwa Daruesh Saliboko na lile la kuweka  usawa lilifungwa na Salum Chubi dakika ya 90. 


Kagera Sugar 3-1 Coastal Union, Uwanja wa Kaitaba.Coastal Union walianza kupachika bao dakika ya 45 kwa mkwaju wa penalti uliofungwa na Abdul Suleiman. Kagera Sugar walipindua kupitia kwa Nassoro Kapama dakika ya 56,Peter Mwalyanzi dakika ya 73 na msumari wa mwisho ulipachikwa na Sadat Mohamed dakika ya 80.


Biashara United 3-0 Mbeya City,  Uwanja wa Karume. 

Mabao ya Biashara United yalifungwa na Christian Zigah dakika ya 10 na 25 na lile la mwisho lilipachikwa na Derick Mussa dakika ya 68.

Mchezo unaofuata usiku saa 1:00 ni Azam FC  v Ruvu Shooting,  Uwanja wa Azam Complex.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic