KIRAKA wa Klabu ya Simba, Erasto Nyoni amefunguka kuwa anaamini timu hiyo itaibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa ugenini dhidi ya Klabu ya FC Platinum unaotarajiwa kupigwa Desemba 23, Harare, Zimbabwe.
Simba tayari imewasili Jijini Harare leo Desemba 18 kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo wa raundi ya kwanza ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.
Simba imefuzu hatua hiyo baada ya kuwaondosha Klabu ya Plateau United ya Nigeria kwenye mchezo wa raundi ya awali.
Akizungumza kuhusu mchezo huo Nyoni amesema: "Tunatumaini utakuwa mchezo mgumu kutokana na ubora wa wapinzani ambao tunakwenda kukutana nao.
"Lakini Wanasimba wanapaswa kutuamini na kuendelea kutuombea kwani tunaenda kwenye mapambano na naamini tunakwenda kushinda mchezo huu,".
0 COMMENTS:
Post a Comment