AISHI Manula, kipa namba moja wa Klabu ya Simba amesema kuwa wamekubaliana kufanya makubwa kwenye michuano ya kimataifa jambo linalowapa matumaini ya kupata matokeo kwenye mechi zao.
Simba ilipenya kimataifa baada ya kushinda mchezo wa awali dhidi ya Plateau United ya Nigeria uliochezwa Uwanja wa New Jos, Nigeria, Uwanja wa Mkapa, Desemba 5 zilitoshana nguvu bila kufungana jambo lililoipa faida Simba.
Ndani ya dakika 180 kwenye mechi za kimataifa Manula alikuwa shujaa kwa kulinda lango lake liwe salama kwa kuwa hakufungwa.
Akizungumza na Saleh Jembe, Manula amesema kuwa wana kazi kubwa ya kufanya kimataifa na wanaamini watafanya vizuri.
”Tumekubaliana wachezaji kufanya makubwa kimataifa na hilo lipo wazi kwa kuwa nafasi tunayo kwa sasa. Imani yetu ni kwamba tutapambana ndani ya uwanja katika kutafuta matokeo.
“Ushirikiano ni mkubwa na hatua ambayo tupo kwa sasa ni kubwa pia hilo lipo wazi, tunakwenda kupambana na benchi la ufundi wameona namna itakayotupa matokeo chanya,” amesema Manula.
Hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba itacheza na FC Platinum ya Zimbabwe Desemba 23
Leo Desemba 18 kikosi kimewasili nchini Zimbabwe kwa ajili ya mchezo wao wa kimataifa na mchezo wa marudiano unatarajiwa kuchezwa kati ya Januari 5-6.
0 COMMENTS:
Post a Comment