KOCHA Mkuu wa Ruvu Shooting, Charles Mkwasa amesema kuwa kikosi chake kipo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC.
Ikiwa nafasi ya nne na pointi 24 inakutana na Azam FC iliyo nafasi ya tatu na pointi 28 Uwanja wa Azam Complex zote zikiwa zimecheza michezo 15.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mkwasa ambaye kwa msimu wa 2020/21 ni wa kwanza kutwaa tuzo ya kocha bora kwa makocha wazawa amesema kuwa wanatambua utakuwa mchezo mgumu ila wanahitaji kupata pointi tatu.
“Utakuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani tumejipanga kupata matokeo,kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kwani kila timu inahitaji matokeo nina amini tutafanya vizuri,” amesema.
Azam FC itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kulazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na Namungo FC Uwanja wao wa nyumbani, Azam Complex.
0 COMMENTS:
Post a Comment