December 20, 2020


INGIZO jipya ndani ya Klabu ya Yanga Mrundi, Saido Ntibazonkiza ‘Saido’ amefunguka kuwa anaona kabisa msimu huu atakuwa sehemu ya kikosi hicho kitakachotwaa ubingwa.

 

Saido alisema amegundua kuwa Yanga ni moja kati ya timu bora yenye wachezaji wenye uchu wa kutaka mafanikio ndiyo maana kila mchezo wanaocheza huwa wanajitoa kwa asilimia 100 na kupambana hadi mwisho kuhahakisha ushindi unapatikana.


Jana, Desemba 19 Uwanja wa Sheikh Amri Abeid ilikuwa ni mchezo wake wa kwanza ndani ya ardhi ya Bongo kwenye Ligi Kuu Bara.

 

Wakati Yanga ikishinda mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji alitupia bao moja na kutoa pasi moja ya bao kwa Bakari Mwamnyeto.


Saido amesema: “Wakati nakuja hapa sikuwa nafahamu kiundani nitakutana na watu wa aina gani, kiukweli nimehamasika sana baada ya kukuta kila mtu ndani ya Yanga analia na ubingwa, hiyo imepelekea kwenye kila mchezo wachezaji kujitolea hadi mwisho.

 

"Hali hiyo imenifanya hata mimi sasa kutamani kuipa ubingwa timu hii na Mungu akipenda msimu huu tutakuwa mabingwa," .


Mchezo wa kwanza wa kirafiki, Saido alifunga mabao mawili ilikuwa Uwanja wa Liti wakati timu hiyo ikishinda mabao 3-1 dhidi ya Singida United ambayo watakutana nayo hatua ya tatu, mchezo wa Kombe la Shirikisho.

7 COMMENTS:

  1. Ubingwa wa kuongea na kwenye magazeti mtaupata

    ReplyDelete
  2. Kaongea nini cha kuwakera watu siku zote timu kubwa huwa zina ndoto za kuchukua ubingwa hilo hakuna kipingamizi ila kma yanga nayo ni level za biashara, coastal,kagera na nyngne basi mna haki ya kukerwa na mbio za ubingwa na kuzungmzia ubingwa. n ivo tu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic