December 20, 2020

 


BENCHI la ufundi la Klabu ya Simba, leo Desemba 20 wamekagua Uwanja wa Taifa wa Zimbabwe ambao utatumika Septemba 23 kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya FC Platinum.


Kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck raia wa Ubelgiji na msaidizi wake Seleman Matola ambaye ni mzawa kimeshapiga kambi nchini Zimbabwe.

Desemba 18 kiliwasili nchini humo ikiwa ni hesabu za Sven katika kutaka kikosi kiweze kuzoea mazingira ya ugenini.

Kocha huyo ameweka wazi kwamba wana kazi kubwa ya kufanya ugenini ili kusaka ushindi kwa kuwa lengo ni moja kushinda ili kutinga hatua ya makundi.

"Malengo yetu ni kuona kwamba tunashinda na kupata matokeo mazuri kwenye mchezo wa kwanza kisha ule wa marudio nao tutapambana kusaka ushindi.

"Wapinzani wetu ni timu kubwa na imara ila haitupi mashaka kwa kuwa nasi pia tupo imara," .

4 COMMENTS:

  1. Safi uongozi, Simba nikioo tufanye vzr tuwafhndishe wdg zetu mafanikio yakisoka

    ReplyDelete
  2. Tunawapongeza sana kwa Kitendo cha Kwenda Mapema Zimbabwe, kitendo cha kukagua Uwanja mapema pia ni mbinu nzuri sana. Tunaimani na uongozi wa Simba, Benchi la Ufundi, Wachezaji wote wa Simba.Tunaendelea kuomba dua kwaajili ya Mchezo huo Muhimu kwa Taifa letu la Tanzania.

    ReplyDelete
  3. Uongozi umefanya vya kutosha na iliyobaki ni timu kuwajibika nasi wapenzi yupo nyuma yenu na Mungu yupo pamoja nasi sote

    ReplyDelete
  4. Mungu Ibariki Simba ipate ushindi ili kuendelea kwenye hatua inayofuata. Ushindi wa ugenini ni muhimu sana, mmeona jinsi figisu kwenye mechi ya marudiano na ndugu zetu wa Nigeria.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic