December 30, 2020

 


LIGI Kuu Tanzania Bara ikiwa inaingia mzunguko wa pili yamefungwa jumla ya mabao 267 huku timu yenye mabao mengi ni Simba.

Kinara wa kutupia mpaka muda huu ni John Bocco akiwa amefunga mabao 8 ndani ya Klabu yake ya Simba.

Nyota 12 wametupia mabao manne kibindoni ambapo kinara wao ni Lamine Moro wa Yanga ambaye yeye ni namba moja kwa mabeki wa Bongo kwa kucheka na nyavu. Ametupia mabao manne kati ya 28 yaliyofungwa na timu hiyo inayoongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 43.

Wengine ni Yacouba Songne mshambuliaji wa kikosi cha Yanga.

Michael Sarpong wa Yanga katika mabao hayo manne moja aliwatungua watani zake Simba kwa mkwaju wa penalti, Uwanja wa Mkapa.

Deus Kaseke wengi wanapenda kumuita mwaisa kiraka wa Yanga.

Bigirimama Blaise ni kinara wa utupiaji ndani ya Namungo na alikuwa ni nyota wa kwanza kutupia msimu wa 2020/21 aliwatungua Coastal Union.

Kibu Denis wa Mbeya City ni namba moja kwa kucheka na nyavu kwenye kikosi hicho.

Relliants Lusajo wa KMC ni namba moja kwa kucheka na nyavu.

Yusuph Mhilu wa Kagera Sugar ni namba moja kwa kucheka na nyavu ndani ya kikosi hicho. 

Daniel Lyanga wa JKT Tanzania ni namba mbili kwa kucheka na nyavu ndani ya kikosi hicho.

Raizin Haji wa Coastal Union ni namba moja ndani ya kikosi hicho cha Juma Mgunda.

Ayoub Lyanga wa Azam FC ni namba mbili kwa kucheka na nyavu.

Obrey Chirwa wa Azam FC naye pia ni namba mbili ndani ya Azam FC.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic