December 29, 2020

 


KOCHA wa zamani wa Klabu ya Simba, Jamhuri Khwelu maarufu kama Julio amesema kuwa suala la nidhamu kwa mchezaji ni jambo la msingi.


Maneno hayo ameyasema ikiwa ni baada ya kiungo wa Simba, Jonas Mkude kusimamishwa ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck.


Mkude amesimamishwa kwa muda kupisha uchunguzi wa tuhuma ambazo anatajwa kukutwa nazo za utomvu wa nidhamu.

"Nidhamu ni jambo la msingi kwa kila mchezaji hivyo ni ngumu kwa mafanikio ndani na nje ya uwanja kupatikana hivyo kwa walichokifanya Simba naona ni sawa japo ni maamuzi magumu.


"Jambo la msingi kwa mchezaji ni lazima awe na nidhamu ili kufikia mafanikio. Matumaini yangu ni kwamba watakaa na kuzungumza ili waweze kuyamaliza haya.

"Ukweli ni kwamba wengi wamekuwa na hofu kuhusu kukosekana kwa Mkude kwenye mchezo dhidi ya FC Platinum hilo ni jambo la kawaida ndio maana wakati mwingine wachezaji wanaumwa wanakuwa nje ya mpango wa mwalimu.

"Unapozungumza kuhusu timu unazunguzia wachezaji wote ambao wamesajiliwa na timu na sio mchezaji mmoja pekee," .

8 COMMENTS:

  1. Huwezi kuwa na familia bora,halafu mzazi unashindwa kusimamia nidhamu kwa familia yako na wewe mwenywe.!!

    ReplyDelete
  2. Hili sio tamko la Simba ni maoni ya Jamhuri Kihwelo acheni kufinyanga mambo

    ReplyDelete
  3. Mbona kichwa cha habari kinatofautiana na yaliyomo ndani? Hebu fateni weledi na ulumbi wa tasnia ya habar

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wanaweka kichwa cha habari kitakachovutia wasomaji ingawa habari yenyewe haiendani na kichwa cha habari....ni mchezo uliozoeleka kwenye blog hii!!!

      Delete
  4. Hilo tamko ni lako ww na bosi wako salehe sio simba acha unafiki unatumwa na hao vuyura wenzio?

    ReplyDelete
  5. Hivi mbona mnaenda kuchezea akili za watu hivi Hilo ni tamko la uongozi wasimba au ni maelezo ya mtu binafsi

    ReplyDelete
  6. Kwanini heading isiwe Julio atoa tamko,,huu uandishi wenu ni wa kizwazwa

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic