December 18, 2020


 

Taasisi ya watu wanaougua uti wa mgongo nchini (KASI) wameomba nao wakumbukwe kwenye fursa za ajira zinapotokea nchini.

Kauli hiyo imetolewa jana na Katibu mkuu wa KASI, Abdulazizi Shambe wakati wakipokea msaada wa mahitaji mbalimbali ya kibinadamu na pesa taslimu kutoka kampuni ya kubashiri ya Meridian Bet.


Alisema Taasisi yao ina wanachama 1300 kote nchini na miongoni mwao wapo vijana wasomi wenye uwezo wa kuajiriwa lakini wengi wao wanakutana na changamoto za kukubalika katika ajira wakiomba.


"Tunao madereva, walimu, wana habari na hata mimi na leseni B ya ukocha ya UEFA ambayo nilisoma nchini Sweden mwaka 2001 hadi 2003 kabla ya kuanza kuugua.


"Mkurugenzi wetu taifa (Goodwill Linus) ana degree ya uandishi wa habari, mzee wetu kwenye Taasisi, Mohammed Tega ni dereva mzuri wa maroli, ila wapo wengi wenye taaluma mbalimbali ingawa wachache sana ndio wanapata ajira akiwa mwalimu Furaha Mbilinyi anayefundisha Shule ya msingi Lugalo," alisema.

Alisema wamekuwa na changamoto nyingi, kwani baadhi ya waajiri wanashindwa kuwapa watu wenye changamoto hiyo wakihofia namna ya kuwahudumia, lakini Abdulazizi amesema wao wanapokuwa kazini jambo ambalo waajiri hawalifahamu ni kwamba wakiingia eneo la kazi hawatoki hadi muda wa kazi uishe.


"Hiyo ni faida ambayo waajiri wengi hawaielewi wanapoajiri mtu anayeugua uti wa mgongo," alisema huku akiwashukuru Meridian Bet kwa sapoti yao ambayo amesema imewapa faraja na kuona bado kuna jamii inawakumbuka watu wenye tatizo hilo.


Meridian Bet iliwakabidhi vyakula mbalimbali ikiwa unga, sukari, mafuta na vitu vingine vya mahitaji ya kibinadamua, sanjari na pesa taslimu kwa ajili ya kuendeleza taasisi hiyo iliyoanzishwa mwaka 1991 na kusajiliwa mwaka 1997.


Meneja uendeshaji mwandamizi wa Meridian Bet, Carlo Njatu alisema wamelazimika kutoa mkono wa faraja kwenye Taasisi hiyo ili kuwafariji na kuendelea kusaidia jitihada za Taasisi hiyo kama ambavyo sera ya kampuni yao inataka.


"Meridian Bet imekuwa ikishiriki katika kusaidia jamii pia, ukiachana na kazi ambazo imekuwa ikifanya za michezo ya kubashiri, imekuwa ikirudisha kwa jamii na kutoa mkono wa faraja kwa wahitaji," alisema.


Alisema mwaka huu wametoa misaada mbalimbali ikiwamo kusaidia hospitali ya wazee kinyerezi, wagonjwa wa kansa wanaotibiwa Ocean Road Hospitali, walemavu wa ngozi (Albino) Kigamboni, waathirika wa dawa za kulevya Kigamboni, kushiriki kusaidia upimaji macho bure na kutoa miwani kwa waliotakiwa kutumia jijini Dar es Salaam, tukio lilifanyika kwenye hospitali ya jeshi Temeke na sapoti mbalimbali kwa wahitaji wakiongozwa na Mkurugenzi wa Meridian Bet, Chetan Chudasama

Mwandishi Wetu

 

5 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic