December 18, 2020


IMEFAHAMIKA kuwa mastaa wakubwa kunako soka Cristiano Ronaldo na Lionel Messi walimpigia kura, Robert Lewandowski aliyeibuka mshindi wa kinyang’anyiro cha mchezaji bora wa mwaka wa FIFA kwa upande wa Wanaume.

Lewandowski ameshinda tuzo hiyo kupitia mchakato wa kura zilizopigwa na makocha, manahodha wa timu za taifa pamoja na baadhi ya waandishi wa habari za michezo.

Kwa kuwa nyota hao wote ni manahodha kwenye timu zao za Taifa nao walihusika katika upigaji kura hizo.

Ronaldo alimchagua Lewandowski katika nafasi ya kwanza, Messi kwenye nafasi ya pili na kumalizia na Kylian Mbappe, huku Messi yeye akimchagua Neymar Junior kwenye nafasi ya kwanza, Mbappe nafasi ya pili na kuimalizia na Lewandowski kwenye nafasi ya tatu.

Lewandowski ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwa na msimu mzuri uliopita akifanikiwa kufunga mabao 60 kwenye michezo 52 aliyocheza kwenye michuano yote.

 Taarifa iliyotolewa na FIFA kwa kuonyesha namna ambavyo kura zilipigwa imeonyesha kwamba nyota wa Argentina, Messi alimchagua namba moja kwamba ni Neymar, Kylian Mbappe kuwa ni namba mbili na tatu alidondosha kwa Lewandowsk.


 

1 COMMENTS:

  1. Kabebwa coz kiwango chake ni kama akina kane na son
    Na ndio maana walimtoa neymar mapema ili ashinde.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic