December 16, 2020


 YACOUBA Songne nyota wa Klabu ya Yanga ameweka rekodi yake ndani ya msimu wa 2020/21 kwa kuwapoteza nyota wawili tegemeo ndani ya Simba, Clatous Chama na Luis Miquissone, katika kuhusika na mabao mengi ndani ya mchezo mmoja.

 

Nyota huyo amezifuta rekodi za Chama na Luis ambazo waliziweka Uwanja wa Mkapa wakati wakiwa na timu zao ambapo walihusika kwenye mabao matatu huku yeye akihusika kwenye mabao manne ndani ya dakika 90.


Chama na Luis ambao wanacheza ndani ya Simba walianza kuweka rekodi hiyo kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Wakati Simba ikishinda mabao 4-0 dhidi ya Biashara United, Chama alifunga mabao mawili na kutoa pasi moja na kumfanya ahusike kwenye mabao matatu.

 

Luis yeye anashikilia rekodi ya kutoa ‘hat trick’ ya asisti ambapo alitoa jumla ya pasi tatu kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Biashara United uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Septemba 20.

 

Songne mwenye rasta za kubana kichwani alifuta rekodi hizo, Desemba 12 ambapo aliandika rekodi ya kibabe akiwa nje ya Dar, Uwanja wa Kambarage kwa kufunga mabao mawili na kutoa asisti mbili na kumfanya ahusike kwenye jumla ya mabao manne wakati Yanga ikishinda mabao 5-0 dhidi ya Mwadui FC.


Ushindi huo unaifanya Yanga iweze kuweka rekodi kwa msimu wa 2020/21, kupata ushindi mkubwa ndani ya uwanja kwa kuwa mchezo wa mwisho kushinda mabao mengi msimu huu ilikuwa ni wa mabao 3-0 dhidi ya Coastal Union.

 

Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 37 baada ya kucheza mechi 15, ikiwaacha Simba kwa jumla ya pointi 8 ambao wamecheza mechi 13 na pointi zao 29.

10 COMMENTS:

  1. FALA KWELI WEWE MWANDISHI, CHAMA AMEPIGA ASSIST 7 NA KUFUNGA MABAO 6 HUYO MBWIGA MFUGA MIRASTA ANAANZAJE KULINGANISHWA NA HAO ULIOWATAJA? UNAJUA LUIS KAPIGA ASSIST NGAPI? PUMBAVU WEWE

    ReplyDelete
    Replies
    1. shida uelewa umeambiwa katika mechi 1

      Delete
    2. Ukiwa mkia uelewa unakua mdogo sana, hapa mwandishi anazungumzia game moja. Wewe unakurupuka na ku comment ujinga.

      Delete
  2. Natafuta kuona alivyowapoteza namalizia kuona otopolo tu waandishi tuoneeni huruma wasomaji wetu 😂

    ReplyDelete
  3. Unaandikaje rekofi kwa kutumia kigezo cha mechi moja?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Uelewa mbona shida? Kuna rekodi za mechi moja na za jumla ya mechi...mikia kulalama mnatia aibu

      Delete
  4. Mwandishi anaandika kuwanadi utopolo maana kwenye anga la soka wamepotea hivyo anafanya kuwaandika Mara kwa Mara kuwasifia angalau kuwafariji.
    *Wanasimba sisi vitu uwanjani vinaonekana utopolo acha wanadiwe kwenye maandishi*

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sisi tuko kimataifa hao wa hapahapa na waandishi wao wanajazana ujinga

      Delete
  5. Mtatafuta mpaka rekodi za dk 45 ilimradi tu kuwabeba Utopolo... Mpira uwanjani sio magazetini

    ReplyDelete
  6. Type na rekodi za kukosa mabao za uto mwenzio

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic