January 2, 2021


 ALIYEKUWA Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi ya Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Elias Mwanjala imeelezwa kuwa amefungiwa na Serikali kujihusisha na soka.

 

Mwanjala kupitia kamati hiyo iliamuru kuwa mkataba wa kiungo mshambuliaji raia wa Ghana, Bernard Morisson na Yanga ulikuwa na mapungufu kadhaa.

 

Ikumbukwe Yanga ilidaiwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili Morrison jambo ambalo alikana na kuwashtaki Yanga TFF kwa madai kuwa hakuwa ameongeza mkataba huo.

 

Hata hivyo siku chache kabla ya hukumu kutolewa, Morrison alitambulishwa kwenye kurasa za kijamii za Simba akisaini mkataba wa miaka miwili na mashabiki wa Yanga kuona kama Mwanjala alihusika kumpeleka mchezaji huyo kwa wapinzani wao, Simba.


 

Taarifa zimeeleza kuwa Mwanjala amevuliwa vyeo na nyadhifa zake zote katika michezo kwa kipindi cha miaka miwili.

 

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa kiongozi huyo ameondolewa nyadhifa hizo baada ya kupatikana na hatia ya kutwaa madaraka kinyume na utaratibu.

 

“Yule aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya TFF iliyoamuru kuwa mkataba wa Morrison una upungufu na Simba kumchukua mazima amekutana na adhabu kubwa kutoka Serikali.

 

“Mwanjala amevuliwa vyeo na nyadhifa zake zote kwenye michezo na kufungiwa kujihususha na uongozi wowote wa michezo kwa miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kutwaa madaraka kinyume na utaratibu.

 

“Tayari Mwanjala amepewa barua kutoka Serikalini kwenye Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Michezo nchini iliyokuwa chini ya Malangwe Mchungahela, ambapo kiongozi huyo amepewa adhabu hiyo kwa kukiuka Katiba ya Chama cha Soka cha Mbeya, ile ya TFF na FIFA.

 

"Na Serikali imeshawapa nakala ya uamuzi huo TFF kama waajiri wa Mwanjala,” alisema mtoa taarifa huyo.


Alipotafutwa Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo kuzungumzia hilo alisema kuwa: “Watafutwe Chama cha Soka cha Mbeya wazungumzie, sisi hatujapata taarifa hiyo na kama tukiipata tutaitoa kupitia njia zetu rasmi za kutoa taarifa.”


Chanzo:Championi

10 COMMENTS:

  1. Hii habari ina ukakasi mwingi,serikali inahusika vipi na maamuzi ya TFF wakati inafahamika wazi kuwa FIFA inakataza serikali kuingilia vyama vya soka katika uendeshaji na utoaji maamuzi wa mambo ya soka

    ReplyDelete
  2. Huyu mwandishi ni kanjanja kwelikweli. Basi karibu kufikiri kwamba habari inasomwa na wengi wakiwemo wasomi.

    ReplyDelete
  3. Mwandishi anafanya jambo la kijinga sana. Ana insinuate kwamba Mwanjala ameondolewa kwa kumpitisha Bernard Morrison wakati kesi hiyo haihusiki kwa lolote na adhabu aliyopewa.
    Hata kichwa cha habari kimeandikwa ili msomaji apate picha hiyo.
    Ni ukanjanja na kukiuka ethics za journalism.

    ReplyDelete
  4. Kwenye ya Morrison hapa ni Simba na Hans Pope msituzuge

    ReplyDelete
  5. Fanya utafiti ndo ulete habr we mwandishi

    ReplyDelete
  6. Waandishi wakitukanwa wanalalamika, lakini wanatumika hadi aibu. Anataka kujenga taswira kuwa amefungiwa kutokana na kumpeleka morrison simba wakati suala lake ni la huko mbeya

    ReplyDelete
  7. Mwandishi umeandika kishabiki mno kuliko kuzingatia weledi.Inaonesha ni jinsi gani hujali wasomaji Ila unajali hisia zako huo ni ujinga mtupu. Habari imejaa suala la morison wakati mtu kasimamishwa kwa suala jingine

    ReplyDelete
  8. Kimeo siku zote atabaki kuwa kikao... ametajwa hivyo ili tusijiuluze ni nani?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic