UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa kwa sasa akili zao ni kwenye Kombe la Mapinduzi ambalo linatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 5.
Kikosi cha Azam FC kinachonolewa na George Lwandamina kinatarajiwa kutia timu Visiwani Unguja, Januari 4 na kitakuwa na mchezo Januari 5.
Michuano ya Kombe la Mapinduzi inatarajiwa kuanza Januari 4-13 na bingwa mtetezi ni Klabu ya Mtibwa Sugar ambayo iliinyosha Simba kwa bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali msimu wa 2020.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema:"Azam FC tumepangwa Kundi C, sambamba na timu za Mlandege na Malindi, zinazotokea visiwani humo.
"Mechi yetu ya kwanza, itakuwa dhidi ya Mlandege, itakayofanyika Januari 08, saa 10.15 jioni huku tukimalizia hatua ya makundi kwa kukipiga na Malindi Januari 10, saa 2.15 usiku, mechi zote zitafanyika Uwanja wa Amaan.

"Wachezaji wapo vizuri na kila mmoja anahitaji kuonyesha kile ambacho anacho hivyo mashabiki watupe sapoti katika kufikia malengo ambayo tumejiwekea," amesema.
Tunaimani timu yetu itafanya vizuri
ReplyDelete