January 3, 2021

 


BAADA ya kuenea kwa tetesi nyingi juu ya usajili wa straika mpya wa Yanga, raia wa Congo, ambaye ni mchezaji wa zamani wa timu ya Angers ya Ufaransa, Ferebory Dore, anayetajwa kama pacha wa Said Ntibanzokiza ‘Saido’ anatarajia kutua nchini na kujumuika na kikosi hicho tayari kwa kuanza kazi.

 

Tayari Yanga wanadaiwa kumalizana na Dore kupitia kwa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Yanga, Injinia Hersi Said ambaye tayari ameshamaliza biashara na vibali vya mchezaji huyo, Dore mwenye umri wa miaka 31, akitokea Brazzaville, Congo.

 

Dore hadi anaingia rada za Yanga ni mchezaji huru pamoja na huko nyuma kuwahi kukipiga katika Klabu ya Angers ya Ufaransa.

 

Chanzo chetu makini kimeeleza kuwa, tayari Hersi amemaliza dili hilo na muda wowote kuanzia sasa ataanza kuchapa kazi hiyo hivi karibuni.


Kwa sasa kila kitu kuhusiana na mchezaji huyo kimekamilika na kitu kikubwa ambacho kinasubiriwa ni muda tu wa kutambulishwa nyota huyo.

 

"Viongozi tayari wamemaliza kila kitu kuhusiana na vibali vyake na sasa ni yeye tu kujumuika na wenzake kwa ajili na kuanza kucheza,” kilisema chanzo hicho.

 

Hivi karibuni Injinia Hersi aliweka wazi kuwa wapo kwenye mazungumzo ya mwisho na mchezaji ambaye atakuja kuingia moja kwa moja kikosini jambo ambalo sasa limeanza kujidhihilisha kutokana na taarifa hizi.

 

Chanzo:Championi

9 COMMENTS:

  1. Haya majembe ya Yanga ya kila wakati yasiyokwisha wala yasiyokuwa na hesabu mwisho wake yatawaumiza

    ReplyDelete
  2. Tangia wameanza kusajiri hayo majembe ya kulimia ama vipi uatakuwa 100 sasa

    ReplyDelete
  3. Saleh jembe mliutarifu umma kuwa jembe linalotua yanga ni mbombo na mlikuwa na uhakika,leo tena chanzo chenu makini kinaripoti kuhusu jembe jipya ferebory Dore...mnavizia Sana

    ReplyDelete
  4. Ripoti zinaonesha Majembe makali ya Africa mwaka huu yote ni mali yanga

    ReplyDelete
  5. Yaani majority ni mikia imecomment hapa wakati issue sio yao chomoeni Cha chikwende kama inawauma na bado tunachukua wote hao hata huyo Mkude tunajua ni YANGA damu hatushindwi au mnabishaaa waone kwanzaaaa vimikia vimefyata wazim haooo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Waambie hao Mapaka FC/Washirikina FC/Mbumbumbu FC/Mikia FC na majina mengine meengi yanayofanana na hayo

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic