January 12, 2021

 


BEKI na nahodha wa kikosi cha klabu ya Yanga, Lamine Moro anatarajia kurejea nchini wiki hii baada ya kumaliza ruhusa maalum ya kwenda nchini kwao Ghana kutokana na sababu za kifamilia.

Lamine aliondoka nchini Jumatatu ya Januari 4, mwaka huu baada ya kupewa ruhusa ya wiki moja na uongozi wa klabu hiyo ili aweze kwenda kujumuika na familia yake iliyopo nchini Ghana.

Nyota huyo amekuwa muhimili mkubwa wa matokeo mazuri ya Yanga msimu huu, ambapo ukiachana na mchango wake mkubwa katika uimara wa safu ya ulinzi ya Yanga pia ameifungia klabu hiyo mabao manne hivyo mpaka sasa kuwa kinara wa ufungaji kwa wachezaji wanaocheza katika nafasi ya ulinzi.

Akizungumzia ruhusa ya nahodha huyo meneja wa kikosi cha Yanga, Hafidh Saleh amesema: "Nahodha wa kikosi chetu, Lamine Moro anatarajia kurejea nchini wiki hii kufuatia kumaliza muda wake wa likizo ya wiki moja aliyopewa na uongozi kwa ajili ya kwenda kujumuika na familia yake iliyopo kwao Ghana baada ya kushindwa kuonana nayo kwa muda mrefu.

1 COMMENTS:

  1. Anasajiliwa upya? Angalieni namna ya kuandika vichwa vya habari

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic