January 2, 2021


 ADAM Adam, nyota wa JKT Tanzania ambaye jina lake lipo kwenye orodha ya nyota wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kinachojiandaa na Chan  anashikilia rekodi ya kuwa nyota wa kwanza kufunga hat trick ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara.


Msimu wa 2020/21 aliwatungua Mwadui FC Uwanja wa Mwadui Complex wakati JKT Tanzania ikifunga mabao 6-1.


Ndani ya JKT Tanzania ambayo imefunga jumla ya mabao 18 amehusika kwenye mabao nane akifunga saba na kutoa pasi moja ya bao.

Mzawa huyu chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Abdalah Mohamed,’Bares’ hawa hapa walikutana na balaa lake:-

Bao 1, alifunga mbele ya Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba, Mwadui FC aliwafunga mabao 3, Uwanja wa Mwadui.

Namungo FC,aliwafunga mabao 2 Uwanja wa Majaliwa na bao lake la saba alifunga mbele ya Biashara United kwa mkwaju wa penalti.

3 COMMENTS:

  1. Kocha wa taifa stars hana washauri au anao washauri lakini wanamshauri vibaya. Kuna tatizo gani kuchukua magoli kipa watatu wenye uzoefu na mmoja kinda? Utamuachaje khasani Dilunga na uzoefu wake wa mashindano makubwa? Dilunga ndie alietoa mchango mkubwa kabisa hadi Simba kufika robo fainali klabu bingwa Africa.Na Kama kweli kocha analengo la kuandaa taifa stars imara ya baadae vipi anamuacha Ibrahim Aame anamchukua Agrey Moris wakati Azam ni miongoni mwa timu yenye beki tepe tepe kwenye ligi kuu.Ninachokifahamu Mimi timu yetu ya CAN ndio timu yetu ya kombe la dunia na ni timu yetu ya mashindano ya kombe la mabara ya Africa kwani hatuna professional wengi. Maproffesional wetu wengi Tanzania wanatokea Simba ndio timu yenye wachezaji wengi walio na uzoefu wa mechi za kimataifa.Hata wale wanaoshangaa Erasto Nyoni kucheza vizuri taifa stars ni vilaza kwani kwa mchezaji wa Simba kufanya vizuri kimataifa sio Jambo la kushangaa. Hawa wachezaji wa Simba wamekwenda uturuki, South Africa kueka kambi.Wanashindana mazoezini na miongoni mwa wachezaji bora kwenye ukanda huu wa Africa sasa unapoona kocha anapata kigugumizi Cha kumuita mchezaji Kama Mohamed huseni na khasani Dilunga hata muzamiru unajua kabisa mpira wa Tanzaniania utachukua muda kukua kwani huu ndio ule usimba na uyanga aliousema Maguful. Wachezaji wazuri na wenye uzoefu wanaachwa ili kubalanzi kikosi kisionekane Cha Simba. Kocha anaamua kuchukua beki tatu ambao uzoefu wa mechi za kimataifa hamna kabisa.sio kwamba tunazungumza ushabiki bali Kuna ujinga fulani kwenye uteuzi kikosi Cha taifa stars ila shabalala ataendelea kumuabisha kocha wa taifa stars.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha ushabiki Braza heshimu maamuzi ya kocha nadhani hata wewe ungekuwa kocha ungeonesha tu upendeleo,hata maoni yako tu yamejaa upendeleo,hv Tz hii hakuna mchezaji mzuri zaidi ya Dilunga?au beki ya shabalala nchi hii yupo peke yake?bro tumia weledi wa soka ndio uzingumze

      Delete
  2. Acha TZ tutolewe mapema kwenye mashindano yote yanayohusu taifa stars huenda viongozi wa mpira watamtafuta kocha mwenye uchungu na mafanikio na taifa letu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic