January 2, 2021


 KIUNGO mkabaji wa Simba, Jonas Mkude ambaye ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mzawa anayelipwa mshahara mkubwa Bongo.

 

Wakati yeye akiongoza kwa wachezaji wazawa, kiungo mshambuliaji wa timu hiyo, Luis Miquissone raia wa Msumbiji ndiye anayeongoza kukunja mshahara mkubwa kwa wachezaji wageni ambaye yeye anachukua dola 7,000 (zaidi ya Sh 16m) kwa kila mwezi.

 

Inadaiwa kuwa Mkude anakunja Sh 8m kila mwezi tangu alipoongezwa mkataba mwingine wa miaka miwili ya kuendelea kuichezea timu hiyo katika msimu wa 2018/19.


Mkude alipewa mkataba huo baada ya kuwepo tetesi za nyota huyo kuwaniwa na Yanga katika msimu wa 2018 ambapo mkataba wake ulikuwa umemalizika kuendelea kubaki Simba.


Kiungo huyo mwenye uwezo wa kukaba na kupiga pasi fupi na ndefu Desemba 28 alisimamishwa kazi kwa kile kilichotajwa utovu wa nidhamu huku sababu ya kusimamishwa ikifichwa.

 

Cheki ‘Top Five’ ya wachezaji wazawa wanaolipwa mishahara mikubwa katika Ligi Kuu Bara baada ya Mkude kuongoza ambao ni:-


FARID MUSSA.

 

Kiungo mshambuliaji wa Yanga ndiye anayefuatia kwa kuwa inadaiwa anakunja Sh 7m kwa mwezi tangu alipojiunga na timu hiyo katika msimu huu akitokea Tenerife FC ya Hispania.

 

JOHN BOCCO


Nahodha na mshambuliaji wa Simba anashika nafasi ya tatu kwa kulipwa Sh 7m na analipwa kiasi hicho cha fedha baada ya kuongeza mkataba katika msimu wa 2018.

 

Bocco alipewa mkataba huo baada ya kuelezwa kuwa Azam FC walikuwa na mipango ya kumrejesha klabuni hapo.


ERSATO NYONI


Beki na kiungo wa Simba ambaye inadaiwa kuwa analipwa Sh 7m kila mwezi, dili ambalo alisaini mwaka 2018.

 

AISHI MANULA


Kipa namba moja wa Simba naye analipwa Sh 7m kila mwezi, naye dili lake la mwisho la mkataba alisaini mwaka 2018.Manula anapewa changamoto uwanjani na Beno Kakolanya lakini bado Manula ameendelea kuwa chaguo la kwanza kikosini hapo.

11 COMMENTS:

  1. Vipi mnaanika mishahara na huku ikiwa kipato cha mtu ni jambo la siri yake

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ujui chochote kwenye mpira wewe kaa kimya

      Delete
  2. kwenye mpira kipato sio siri mzee, hata ulaya tunajua mishahara ya wachezaji wote

    ReplyDelete
  3. Ronaldo analipwa mabilioni kwa wiki anaweza endesha nchi kama tza lakini anaadabu na heshima na sio mlevi au mpumbavu kama hawa wa kwetu amelelewa na simba nani angemjuwa? Halafu ww mwandishi uchwana huna cha kuandika unaandika ujinga

    ReplyDelete
  4. Huna lolote blog mbovu mbovu kupindukia mkikosa cha kuandika mkaage kimya kuliko kuwa wanafiki

    ReplyDelete
  5. Badilisheni jina owe hata yanga blog kuliko umbea was kishsbiki

    ReplyDelete
  6. Hahahahahah mshahara wa shomari Kapombe huuujui eeeeh

    ReplyDelete
  7. Mkude aende zake tu kwanza yuko slow sana mimi binafsi simkubali mzito sana bana

    ReplyDelete
  8. Wewe acha kupotosha watu,, bocco analipwa mil10+

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic