BAADA ya Azam kukamilisha usajili wa mlinda mlango raia wa
Uganda, Mathias Kigonya, unaweza kusema ‘Wanalambalamba’ hao wamepata jembe kutokana na rekodi za hatari alizonazo nyota huyo.
Kigonya amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea
Azam, amewahi kucheza kwa mafanikio ndani ya Sofapaka na Kakamega za Kenya, Bright Star ya Uganda na Forest Rangers
alipocheza msimu uliopita.
Ametwaa tuzo ya Kipa Bora wa msimu mara
mbili mfululizo wa Ligi Kuu Zambia, msimu wa 2019 (ligi ndogo) na 2019/2020.
Akiwa na kikosi cha Sofapaka ya
Kenya kwa miaka mitatu tangu 2016, Kigonya alifanikiwa kutajwa katika tatu bora ya makipa wa ligi ya Kenya.
Msimu uliopita, hakuruhusu wavu wake kuguswa (clean sheet)
kwenye mechi 14 kati ya 23 alizoichezea Rangers na msimu huu amekusanya nne
katika mechi 10 alizocheza hadi anatua Azam FC.
Mlinda mlango huyo ambaye pia yumo kwenye kikosi cha timu ya
Taifa ya Uganda 'The Cranes', amekuwa na mchango mkubwa akiwa na Forest
Rangers, baada ya kusimama vema akiwa katika milingoti mitatu langoni.
david kisu mlisema haya haya mleteni tutungue sie
ReplyDeleteSapong alikua na record zaidi nzuri yake
ReplyDelete