January 14, 2021

 


UONGOZI wa klabu ya Yanga kupitia kwa Ofisa Mhamasishaji wao, Antonio Nugaz umetamba kufanya utambulisho wa mshambuliaji wao mpya muda wowote kuanzia sasa kama sehemu ya maboresho ya kikosi chao kuelekea kwenye michezo ya raundi ya pili ya Ligi Kuu Bara.

Yanga ambayo Jumatatu ya wiki hii ilikamilisha usajili wa beki wa kati kutoka ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar, Dickson Job akiwa sehemu ya mapendekezo ya kocha Cedric Kaze imekuwa ikihusishwa kwa kiasi kikubwa na baadhi ya mastraika wakiwemo; Fereboy Dore raia wa DR Congo, Kadima Kabangu wa DC Motema Pembe, Steven Sey wa Namungo, Idris Mbombo, Heritier Mkambo wa Horoya na Muivory Coast ambaye wamegoma kuweka wazi jina lake.

Licha ya kuwa na mafanikio makubwa katika michezo yao msimu huu, Yanga wamekuwa na changamoto kubwa katika safu yao ya ushambuliaji, ikijidhihirisha katika michuano ya Mapinduzi ambapo kwenye michezo minne ya michuano hiyo wamefunga mabao mawili pekee tena yakifungwa na viungo.

Akizungumzia mipango ya kumshusha straika huyo Ofisa Mhamasishaji wa klabu ya Yanga, Antonio Nugaz amesema: "Kwanza ni furaha kubwa kwetu kuweza kuibuka mabingwa wa michuano ya kombe la Mapinduzi, tangu kuanza kwa msimu tuliweka wazi kuwa mwaka huu tuna jambo letu na muda wowote kuanzia sasa tunakwenda kumshusha mwamba ambaye ni straika hatari wa mabao ili kuongeza nguvu kwenye safu yetu ya ushambuliaji,"

2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic