January 14, 2021

 



UONGOZI wa Klabu ya Yanga umewatumia salamu za pongezi viongozi wa klabu hiyo Mshauri mkuu, Senzo Mbatha pamoja na Mkurugenzi wa uwekezaji wa wadhamini wa Yanga kampuni ya GSM Injinia, Hersi Said kwa utumishi wao bora ndani ya klabu hiyo.

Yanga walifikisha salamu hizo kupita akaunti zao za kijamii ambapo walichapisha picha ya viongozi hao wawili wakiwa wamebeba kombe la Mapinduzi na kuambatanisha maneno yafuatayo: "Mafanikio huanza na Uongozi bora na madhubuti ama kwa hakika nyinyi ni viongozi wa mfano wa kuigwa katika Klabu yetu.

Chini ya uongozi huo Yanga imefanikiwa kukata kiu ya muda wa miaka mitatu ya kutokutwaa taji baada ya Jumatano ya wiki hii kufanikiwa kutangazwa mabingwa wapya wa michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Simba kwa changamoto ya mikwaju ya penalti 4-3.

Yanga ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze imeshinda mechi mbili mfululizo kwa penalti 4-3 ambapo ilianza kufanya hivyo mbele ya Azam FC hatua ya nusu fainali ya kwanza na hatua ya fainali mbele ya Simba.


Yanga inakuwa imetwaa mataji mawili ya Kombe la Mapinduzi huku Simba ikiwa na mataji matatu kwenye kabati lao la Kombe la Mapinduzi.


10 COMMENTS:

  1. Kwa jinsi Yanga wanavyopagawa na kombe la mapinduzi kiasi fulani ni aibu ila letu jicho. Yaani over celebration on little achievement what nonsense.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni wajinga tu

      Tukitwaa makombe ya maana wataishia kujinyonga hawa utopoli

      Delete
  2. Hivi kumbe miaka mitatu sio kombe la VPL tu, na hata kombe lolote hawakuwa nalo? Eeeh, kumbe afadhali basi wameondoa nuksi kwa Mapinduzi Cup

    ReplyDelete
  3. Asiepata ikitokea amepata dunia nzima itafahamu, ndivyo ilivyo, kuna watu kila siku wanakula pilau, lakini asiyeila, ikatokea amekula kwa bahati, dunia nzima atataka ifahamu nae amekula pilau, kinachofuata wale vumbi tu, hizi kelele tusingeziona pamoja na kero zote

    ReplyDelete
  4. Yani mapinduzi cup ndo linawapagawisha kiasi hicho, nineamini masikini akipata matako hulia mbwata

    ReplyDelete
  5. Mapinduzi cup ndo mtambe hivyo kwanza leteni hilo kombe huku iringa tunywee ulanzi

    ReplyDelete
  6. Zero Short on Target FC

    ReplyDelete
  7. Hii ni aibu nyingine ya Mwaka

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic