January 14, 2021


 


KIUNGO wa zamani wa klabu ya soka ya Yanga na Mbeya City, Raphael Daudi Loth amekamilisha usajili wake wa kujiunga na klabu ya Ihefu ya Mbeya,  na muda wowote kutoka sasa anatarajiwa kutambulishwa rasmi

Loth alijiunga na Yanga mwaka Juni 30, mwaka 2017 na kuichezea mpaka msimu uliopita wa 2019/20 kabla ya kuachwa mwanzoni mwa msimu huu.

Nyota huyo alijiunga Yanga sambamba Mcameroon Youth Rostande kutoka African Lyon, Ramadhan Kabwili kutoka timu B, beki Abdallah Haji kutoka Taifa Jang’ombe, viungo Pius Buswita kutoka Mbao FC, Pappy Kabamba Tshishimbi, Mkongo kutoka Mbabane Swallows ya Swaziland, na mshambuliaji Ibrahim Ajibu kutoka Simba.

Loth pia alikuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichocheza michuano ya COSAFA Castle na kutwaa Medali ya Shaba baada ya ushindi wa penalti 4-2 Julai 7, mwaka 2017 dhidi ya Lesotho kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 90 Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg.

 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic