January 9, 2021

 


AMEZALIWA Septemba 13,1973 ana umri wa miaka 47 ambapo nafasi aliyocheza mwenyewe zama za mpira alikuwa ni beki.

Anaitwa Rene Weiler, raia wa Uswisi aliweka daruga kabatini 2001 alipokuwa anatumikia Klabu ya FC Winterthur.

Anatajwa kuingia rada za Simba kuja kuchukua mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye amebwaga manyanga ghafla.

Sven aliamua kuacha kazi muda mfupi baada ya kupata ushindi mbele ya FC Platinum wa mabao 4-0 na kuipeleka timu hiyo hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.


Ameweka wazi kwamba sababu kubwa iliyomfanya asepe ndani ya kikosi hicho ni masuala ya familia.

Mrithi wake ambaye anatajwa kwa sasa kuja Bongo alikuwa kocha ndani ya Klabu ya Al Ahly ya Misri ila kwa sasa yupo huru baada ya kufutwa kazi Oktoba mwaka jana.


Chanzo:Championi

8 COMMENTS:

  1. Sijui Kama jicho langu linaona Kama viongozi wa Simba au jicho la benchi la Simba linaona Kama Mimi.Punda alikufa kiu huku maji yakiwa kwenye mgongo wake. Simba inahaha kutafuta namba sita au kiungo mkabaji lakini Simba siku nyingi tu wanae kiungo mkabaji au kiungo wa ulinzi ngangari kabisa anaeweza kukomesha kabisa tatizo Hilo kuliko hata Toni lwanga. Kenedi juma.Nimemwangalia nakumfuatilia siku nyingi.Huyu sio mlinzi wa Kati bali ni msaaidizi wa walinzi wa Kati na kazi hiyo anaweza kuifanya kwa ufaha kabisa akawashangaza wengi,anahitaji marekibisho madogo sana. Simba tayari Ina viungo kufunga wengi sana lakini inakosa real defense minded midfielder.
    Kenedi juma akitengenezwa vyema unaweza mfananisha na Fabinho wa Liverpool. Tatizo kwenye timu zetu wakati mwengine huwa tunashindwa kuvibadilisha vipaji na kuvieka kwenye matumizi sahihi tunabaki kukariri na kukomaa kwenye namba ya mchezaji basi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Habari inahusu tetesi za ujio wa kocha mpya we unakuja na habari za kiungo mkabaji.Jaribu kuunganisha maoni yako na habari husika sio kudandia hoja zisizohusiana na mada iliyoandikwa

      Delete
  2. Hiki unachosema kilinifanya nimchukie seven,wachezaji wengi Simba Wana uwezo lakini kocha hakuwa na uwezo wa kuwaongezea kitu kipya na hata kutumia kile walichonacho alishindwa.kahata,ajibu,kenedi juma,ame beki kisiki huyu wote ni wachezaji hatari lkn hawakuwa na kitu mbele ya kocha.hata akina chama walionekana wako vzr ni kwa sabb ya uzoefu wa kujiongeza dimbani.

    ReplyDelete
  3. Wanapoleta kocha waangalie mwenye uwezo wa kukuza hata kipaji Cha mchezaji vinginevo tutakuwa tunasajili kila siku na kuuwa vipaji.huyu kocha anaweza?

    ReplyDelete
  4. mkataba wa kocha ndo humuongiza yy kama ameambiwa ahakikishe timu inashinda kombe fulan we unafikiri atakuwa na nafasi ya kukuza vipaji?

    ReplyDelete
  5. Kocha hakuwa na uwezo wa kuwaongezea wachezaji vitu

    ReplyDelete
  6. Tusidanganyane bhanaa..Huyu kocha CV yake siyo ya kuangaunga na inaonyesha pesa yake ni maji marefu.

    ReplyDelete
  7. Tuwe wakweli kuwa wachezaji wengi viwango vyao vilishuka wakiwa chini ya kocha Sven.Kina Rashid Juma, Mpilipili,Kahata,Kagere,
    Bodi inatakiwa kuwa na mkurugenzi wa ufundi ili awe link na benchi la ufundi na bodi ili kocha asiwe mungu mtu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic