TUPO Januari 4 leo ndani ya mwaka mpya wa 2021 ambao umeanza kwa kasi yake taratibu tunaendelea kuumega mwaka huu kwa Neema ya Mungu.
Ndani ya kurasa ambazo tumezipita kuna mengi ambayo yameandikwa na kuacha kumbukumbu, huku kila kurasa ikiwa na kumbukumbu yake.
Kwenye ulimwengu wa mpira, yapo mengi ambayo yameandikwa na yatabaki kwenye kumbukumbu namna hii:-
Corona
Bado ni janga kwa dunia ambapo iliweza kusimamisha masuala mengi ya michezo pamoja na shughuli za kijamii.
Ligi Kuu Bara ilisimamishwa na Ligi Kuu England nayo pia ilisimamishwa ndani ya mwaka 2020 ambapo iliporejea kulikuwa na umuhimu wa kuchukua tahadhari kwa mashabiki.
Pia michuano ya Afcon ambayo ilitarajiwa kufanyika 2021 imepelekwa mbele mpaka 2022 kwa sababu ya Corona.
Simba ubingwa
Iliweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2019/20 na kufanya ichukue jumla ya mataji matatu na hili likawa lao jumlajumla kabatini.
Pia ilitwaa taji la Kombe la Shirikisho baada ya kuifunga mabao 2-0 Namungo kwenye mchezo wa fainali uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa.
Sakata la Morrison
Mchezaji wa Simba, Morrison sakata la mkataba wake liliweza kuchukua sura mpya ambapo lilisikilizwa kwa muda wa siku tatu makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF).
Ilikuwa ni utata wa mkataba wake ambapo Yanga walikuwa wanadai ni mchezaji wao ambaye amesani dili la miaka miwili huku Morrison akieleza kuwa mkataba wake alisaini dili la miezi sita.
Mwisho hukumu ilitolewa kwamba mchezaji huyo ni huru anaweza kujiunga timu yoyote na alichagua kuibukia Simba ambapo alisaini dili la miaka miwili.
Usajili wa Kichuya
Sakata la Shiza Kichuya nyota wa Klabu ya Namungo liliweza kuwa gumzo baada ya Fifa kuitaka Simba kuwalipa fedha Klabu ya Pharco ya Misri kwa kosa la kumpa mkataba nyota huyo akiwa hajamaliza mkataba wake ndani ya timu hiyo.
Suala hilo limekatiwa rufaa na Simba baada ya kueleza kuwa hawakusilizwa kwenye kesi hiyo.
Simba v Yanga mara nne
Mwaka 2020 umeshuhudia Dar Dabi nne ndani ya ardhi ya Bongo, Uwanja wa Mkapa.
Mchezo wa kwanza ulikuwa ni wa Ligi Kuu Bara, Januari 4 Uwanja wa Mkapa, ngoma ilikamika kwa sare ya kufungana mabao 2-2. Mzunguko wa pili ilikuwa ni Machi 8, Yanga 1-0 Simba na mchezo wa tatu ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho ambapo Simba ilishinda mabao 4-1.
Mara ya nne ilikuwa ni Novemba 11, Uwanja wa Mkapa ulikuwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara ulikamilika kwa sare ya kufungana bao 1-1.
Fungiafungia ya viwanja
Hali haikuwa shwari kwa viwanja vingi ndani ya Bongo ambapo fungiafungia iliwakuta na kuwafanya wahame makazi ya timu zao miongoni mwa viwanja ambavyo vilifungiwa ni pamoja na CCM Gairo na ule wa Jamhuri Morogoro yote inatumiwa na Mtibwa Sugar.
Jamhuri, Dodoma, Mkwakwani wa Tanga,Sabasaba wa Njombe, Ushirika wa Moshi unaotumiwa na Polisi Tanzania.
Vigogo waonja joto ya jiwe
Hali haikuwa poa kwa vigongo ndani ya ligi Bongo ambapo walikutana na joto ya jiwe kwa kutakiwa kulipwa faini na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kutokana na makosa mbalimbali.
Haji Manara, Ofisa Habari wa Simba, alikutana na rungu la kupigwa faini ya milioni tano na onyo la kutofanya makosa ya kimaadili kwa muda wa miaka miwili kwa kitendo cha kuchafua taswira ya TFF kushusu sakata la Bernard Morrison.
Hassan Bumbuli yeye kitendo cha kusema kwamba TFF haijawapa nakala ya kesi ya Morrison ilimponza kwa kuwa alikutana na joto la faini ya milioni tano
Antonio Nugaz, Ofisa Uhamasishaji wa Klabu ya Yanga alikutana na joto la faini ya laki tano baada ya kufanya mahojiano kwenye eneo la kuchezea kwenye mchezo dhidi ya Gwambina FC.
Timuatimua makocha
Falsafa ya kocha kuajiliwa ili afukuzwe kwa mwaka 2020 ilikuwa inaishi kwa kuwa wengi wamefutwa kazi na wanaendelea mishe nyingine.
Zlatko Krmpotic aliyekuwa kocha mkuu wa Yanga alifutwa kazi Oktoba 3 kwa sasa nafasi yake ipo mikononi mwa Cedric Kaze.
Maka Mwalisi wa Ihefu alifutwa kazi Oktoba 6 mikoba yake ipo mikononi mwa Zuber Katwila,Zuber Katwila huyu alibwaga manyanga ndani ya Mtibwa Sugar Oktoba 18 alimuachia mikoba Vincent Barnaba.
Amri Said wa Mbeya City alifutwa kazi Oktoba 21 mikoba yake ipo kwa Mathias Lule, Hitimana Thiery alifutwa kazi Novemba 18 mikoba yake ipo kwa Hemed Morroco, Aristica Cioaba alifutwa kazi Azam FC Novemba 26 mikoba yake ipo kwa George Lwandamina.
Khalid Adam wa Mwadui FC naye pia alifutwa kazi ndani ya kikosi hicho kutokana na mwendo mbovu mikoba yake ipo mikononi mwa Amri Said.
Kifo cha Mkapa
Julai 24,2020 itabaki kwenye kumbukumbu ya familia ya michezo pamoja na dunia kiujumla baada ya Benjamin Mkapa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa miaka 10 kutangulia mbele za haki.
1995-2005 alikuwa madarakani akitoa huduma kwa taifa la Tanzania. Anakumbukwa kwa mchango wake mkubwa kwenye sekta ya michezo ikiwa ni kusapoti timu zote za ndani pamoja na zile za taifa.
Mbali na kuanza kujenga Uwanja wa Taifa wa Tanzania ambao kwa sasa unaitwa Uwanja wa Mkapa inatajwa kuwa alikuwa ni shabiki wa Yanga.Kuondoka kwake kuliacha ganzi kwa taifa kiujumla.
Janja janja ya kuivuruga Simba ... You can fool some people some time but you cant fool them again and again
ReplyDelete