BEKI wa timu ya Yanga, mzawa Yassin Mustapha amesema kuwa jina lake kuitwa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni fahari kubwa na anaamini kwamba atapambana kwa ajili ya taifa bila kuogopa.
Mustapha ni miongoni mwa wachezaji 30 ambao wamechaguliwa na Kocha Mkuu, Ettiene Ndayiragije ndani ya Stars ambayo inajiandaa na michezo mwiili ya kirafiki dhidi ya timu ya Taifa ya Congo.
Beki huyu alitua Klabu ya Yanga akitokea Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Malale Hamsini ila kwa sasa yupo chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze ndani ya Yanga.
Tayari kikosi kimeweka kambi Posta na kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya michuano ya Chan pia.
Mustapha amesema:"Kuwa ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania ni kitu kizuri kwangu kwa kuwa ninafanya kwa ajili ya taifa langu ambalo ninalipenda.
"Kila mchezaji anapenda kucheza ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania nami nafurahi kuwa ndani ya timu kwa wakati huu hivyo mashabiki kitu kikubwa kinachohitajika kwao ni sapoti," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment