LEO ni leo asemaye kesho huwa anatajwa kuwa ni muongo. Huu ni msemo ambao wahenga walitufundisha zama zile wakati wa matatizo makubwa ambayo tulipitia ama katika kusaka ushindi wa namna yoyote ile.
Hatimaye ile siku ambayo inasubiriwa kwa
shauku kubwa na wapenda soka Tanzania imewadia nayo ni leo. Hakuna siku
nyingine tena zaidi ya leo kuwa ni siku ya furaha na pia inaweza kuwa ya huzuni
pia.
Ninasema
hivyo kwa sababu kazi iliyopo mbele ya timu yetu ya Taifa ya Tanzania, Taifa
Stars ni leo kupambana kufikia ndoto zile ambazo zilikuwa zinaotwa na
Watanzania wengi kwa muda mrefu.
Ile ndoto ya
kutinga hatua ya robo fainali ni ndoto ambayo inapaswa itimie leo kwa Stars
kushinda kwenye mchezo wake dhidi ya Guinea hakuna habari nyingine.
Ukweli upo
wazi kwa kila Mtanzania kupenda kuona timu ya Tanzania inafanya vizuri.Na
inawezekana ikiwa kila mmoja akatimiza wajibu wake ndani ya uwanja na nje ya uwanja.
Kwa kundi D
ambalo linaongozwa na Guinea wenye pointi nne sawa na Namibia wenye pointi nne
hapo ina maana kwamba ikiwa timu itapata ushindi kwenye mchezo wa leo inapenya
jumla hatua ya robo fainali.
Nina amini
kwamba wakati huu wa haya mashindano ya Chan wapo ambao watafungua ukurasa wao
mpya wa kutoka katika ulimwengu wa mpira. Njia ni moja tu kwa wachezaji kucheza
kwa juhudi na kusaka matokeo bila kukata tamaa.
Kinachotakiwa
leo kwa wachezaji wote ndani ya uwanja ni kupambana bila kukata tamaa na kusaka
ushindi ndani ya dakika 90 ili kukata tiketi ya kutinga hatua ya robo fainali
inawezekana.
Ni muda wa
kazi ndani ya uwanja kwa kila mmoja hizi dakika 90 ambazo mnazo leo zimeshika
funguo ya furaha kwa mashabiki na funguo ya mafanikio kwa timu ya Taifa ya
Tanzania.
Kuna suala
la timu kupanda viwango kwa Tanzania kiujumla hili ni jambo la msingi na hapa
ndipo ambapo ramani ya mafanikio kwa soka la Tanzania inachorwa leo.
Hakuna
ambacho kwa sasa kinasubiriwa na mashabiki pamoja na taifa kiujumla zaidi ya
kushangilia ushindi wa leo hivyo wachezaji hili ni deni kwenu.
Mkiingia
uwanjani mnapaswa kuwa watulivu na kucheza kwa nidhamu kubwa kwa kuwa ikiwa
mtaingia kwa presha ni rahisi kushindwa kufikia yale ambayo mnayatarajia
kuyafanya.
Yale ambayo
mmepewa na benchi la ufundi ni muhimu kuyafanya ndani ya uwanja na pia ni
lazima kila mmoja aongeze juhudi binafsi ndani ya uwanja. Kazi ni moja
kupambana kusaka ushindi.
Ni wazi
kwamba kila mchezaji anapenda kufanya vizuri lakini asisahau kwamba inacheza
timu wala hachezi mchezaji mmoja hivyo ni lazima wachezaji mpambane huku
mkishirikiana.
Benchi la
ufundi nalo pia kwenye upangaji wa kikosi lipange kikosi cha ushindi ninaona
kwamba ikiwa wataweza kufanya mabadiliko kwenye kikosi pia tutarajie mabadiliko
kwenye matokeo.
Duniani kote mwalimu huwa anakuwa na kikosi
cha ushindi na kuna kikosi ambacho tayari kimeshazoeana kuleta ushindi hapo
akili inahitajika katika kikosi cha leo na wale ambao watapangwa kazi yao iwe
moja kupambana kusaka matokeo ndani ya uwanja.
Wachezaji 11
ni alama tosha ya ushindi leo na umoja wa kila mchezaji ni nguvu ya ushindi
ukichanganya na dua za mashabiki pamoja na wachezaji basi kazi inakuwa
imemalizika.
Ukweli
usiofichika ni kwamba namna ambavyo tunahitaji kushinda hata wapinzani wetu pia
Guinea wanahitaji kushinda. Hapo kinachohitajika ni kitu kimoja juhudi isiyo ya
kawaida kwa wachezaji.
Kikubwa
ambacho wachezaji wanapaswa wakifanye ni kujitambua na kubeba nguvu ya
kujiamini kwamba wanaweza kupata matokeo uwanjani kwa kupambana bila kuchoka.
Jambo la
msingi kwa sasa ni kila mchezaji kujua kwamba anatambua anakutana na ugumu
mkubwa ila furaha yake iwe kwenye kusaka ushindi ndani ya uwanja bila kukata tamaa.
Imani yangu
ni kwamba kila kitu kinawezekana na ushinid upo kwenye miguu yenu hivyo fanyeni
kweli pambaneni bila kuchoka kusaka ushindi tunawaamini wapambanaji wetu.
Kama
wachezaji mtaamua kujituma uwanjani pasipo kumtegemea mchezaji mmoja maana yake
ni kwamba mtapata matokeo mazuri ambayo mnayafikiria.
Ila kama
kila mmoja atakuwa anajiona yeye ni bora kuliko mwingine hapo ndipo tatizo
linapoanzia hasa kwa kufanya ushindani na ule ubora kupotea.
Leo kila
mmoja ni bora na kila mmoja ni mshindi. Imani ni kwamba anayeweza kutetea taifa
letu leo ndani ya uwanja inawezekana na kila mchezaji anaweza kuleta ushindi
kwa ajili ya taifa.
Kila mmoja
akubali kujitoa kwa ajili ya timu na afanye kazi kwa juhudi akiwa
uwanjani.Furaha ya wachezaji ni ushindi na furaha ya Watanzania ni ushindi,
kila la kheri.
Tunaamini
kwamba tunaweza kufanya mapinduzi katika soka letu kwa kupata matokeo na
kuushangaza ulimwengu kwa sababu kila mmoja ni mshindi kwa sasa.
Watanzania
tusisahau pia kuwaombea dua hawa wanajeshi wetu ambao watakuwa kazini kusaka
ushindi. Kila mmoja ana kazi ya kutimiza majukumu yake.
Hivyo ni
muhimu wachezaji wetu kutambua kwamba kazi yao leo iweze kutimia lazima
wapambane kushinda na itawafungulia pia milango ya kupata timu nyingine nje ya
Bongo.
Chan
inafuatiliwa na wengi hivyo kwa wale ambao wanafanya vizuri kazi inakuwa moja
kwa mawakala kuweza kuzungumza nao na kufungua ukurasa wa kufanya nao biashara.
0 COMMENTS:
Post a Comment