January 27, 2021




 EDEM Mortotsi nyota wa zamani wa Klabu ya FC Edmontok yupo kwenye hesabu za mwisho za kumalizana na vinara wa Ligi Kuu Bara, Yanga.

Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 44 baada ya kucheza jumla ya mechi 18 msimu wa 2020/21.

Mortosi mwenye umri wa miaka 27 tayari yupo Dar es Salaam tangu jana kwa ajili kukamilisha dili hilo kabla ya kusaini kandarasi yake na anatajwa kuwa atakuwa kwenye benchi la ufundi. 

Mortotsi alizaliwa nchini Ghana lakini alikulia Edmonton nchini Canada. Alichezea Klabu ya FC Edmonton kwa miaka saba kuanzia Aprili 2013 hadi Desemba 2020.

Msimu wa 2020 hakuwa ndani ya uwanja kuonyesha makeke yake kutokana na majeraha na aliletwa duniani Aprili 16,1993.

4 COMMENTS:

  1. Hongera Yanga kwa kusajili nyota wanaozidi mia. Haya ni maendoleo makubwa hakuna clab yoyote iliyofikiwa na wananchi. Zidini kuchemsha hata tutwae kila kitu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyo ni mchezaji aliyesajiliwa na blog hii na siyo Yanga

      Delete
  2. Nyie wanaume, mbona mnashambulia bila kujua undani wa habari? Mchana anakuja kuwa mtaalamu wa ufundi, si kama mchezaji.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic