KOCHA
mkuu wa klabu ya AS Vita ya DR Congo, Frolent Ibenge amesema kuwa bado
anaukumbuka vizuri mchezo wa kipigo cha mabao 2-1 walichokipata dhidi ya Simba
kwenye hatua ya Makundi msimu wa 2018/19.
Mchezo huo ulikuwa wa mwisho kwa timu
hizo mbili zilizokuwa zimewekwa kwenye kundi D, pamoja na Al Ahly na JS
Saoura ambapo ushindi huo uliwapa Simba tiketi ya kufuzu hatua ya robo fainali
ya michuano hiyo mikubwa kwa ngazi ya klabu Afrika.
Simba iliyokuwa ya kwanza
kufungwa bao kupitia kwa nyota wa AS Vita, Kazadi Kasengu ilijipatia mabao yake
kupitia kwa Mohammed Hussein na Clatous Chama.
Simba imepangwa tena na AS Vita
msimu huu kwenye kundi A, la Ligi ya mabingwa pamoja na Al Ahly pamoja na Al Merrikh ya Sudani.
Akizungumzia kuhusu mchezo huo
Ibenge alisema: "Moja ya mechi ambazo siwezi kuzisahau nikiwa katika ardhi
ya Tanzania ni ile ya kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya Simba nikiwa na AS Vita
katika michezo ya hatua ya makundi msimu wa 2018/19.
"Malengo yetu kwenye
mchezo ule ilikuwa kupata ushindi, lakini tulijikuta
tunapoteza na Simba wakatinga hatua ya robo fainali, msimu huu tutakutana nao
tena na najua haitakuwa rahisi na nilazima tujipange mapema,"
0 COMMENTS:
Post a Comment