BAADA ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya DR Coongo, kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Etienne Ndayiragije amesema kuwa watatumia mbinu mpya kwenye mechi zijazo ili kupata matokeo.
Stars ilianza kufungwa dakika ya 19 kupitia kwa Fiston Mayele dakika ya 19 bao lililodumu mpaka dakika ya 45 baada ya mabeki wa Stars kufanya uzembe kuokoa hatari na kipa mkongwe Juma Kaseja kuteleza kabla ya kuokoa mpira huo.
Pongezi kwa Ditram Nchimbi ambaye aliingia kipindi cha pili akitokea benchi akichukua nafasi ya Adam Adam ambaye aliweza kubadili mchezo kwa kuongeza kasi ya ushambuliaji.
Alitoa pasi
dakika ya 56 iliyokutana na kichwa cha Ayoub Lyanga aliyeijaza kimiani kwa
kichwa na kuwanyanyua mashabiki wa Stars.
Kaseja naye hakumaliza dakika 90 nafasi yake ikichukuliwa na Aishi Manula, Deus Kaseke alimpisha Yusuph Mhilu.
Mchezo wa jana ambao pia ulikuwa maalumu kwa ajili ya kumuaga mkongwe Agrey Moris ambaye alitumia dakika 3 na nafasi yake ikichukuliwa na Karlos Potrels ulihudhuriwa na mashabiki kiasi ambao walijitokeza kuipa sapoti Stars.
Mbali na
kucheza mchezo huo wa mwisho nyota huyo alipewa milioni tano kwa ajili ya
pongezi kwa huduma yake Stras na jezi iliyosainiwa na wachezaji pamoja na
benchi la ufundi.
Ndayiragije amesema:"Bado tuna kazi ya kufanya kwa ajili ya timu kupata matokeo kwenye mechi zake, kwa namna ambavyo wachezaji wamecheza yale makosa yaliyotekea ndani ya uwanja tutayafanyia kazi.
"Ukweli ni kwamba wachezaji wengi walikuwa wapya lakini wamejitahidi kwa namna ambavyo wanaweza kupambana, bado tuna kazi ya kufanya, imani yetu ni kwamba mechi zijazo tutakuwa na mbinu mpya ambazo zitatupa matokeo chanya" .
0 COMMENTS:
Post a Comment