January 11, 2021

 



YANGA inatinga hatua ya fainali ya Kombe la Mapinduzi kwa ushindi wa penalti 5-4.

Yanga itakutana na mshindi wa mchezo wa nusu fainali ya pili kati ya Simba na Namungo.
FT: Yanga 1-1 Azam FC
Hatua ya nusu fainali ya kwanza 
Zinaongezwa dakika 3
Dakika 90 Benedict Haule anaingia anatoka Maseke
Dakika 88 Chirwa anafanya jaribio linaokolewa na Shikalo
Dakika ya 67 Goal Azam FC,Obrey Chirwa
Dakika ya 56 Niyonzima anafanya jaribio linaokolewa na kipa wa Azam FC inapigwa kona inaokolewa
Dakika ya 51 Goal kwa Yanga linafungwa na Tuisila Kisinda kwa pasi ya Haruna Niyo
Dakika ya 45 Chirwa anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Kisinda
Kipindi cha pili kimeanza Uwanja wa Amaan
NUSU Fainali ya kwanza Kombe la Mapinduzi 

Yanga 1-0 Azam FC 

Uwanja wa Amaan


Mapumziko 

Dakika 45 zinakamilika kwa timu zote kutoshana nguvu ngoma inaendelea dakika 45 zijazo

 Dakika ya 38 Yacouba anapeleka mashambulizi Azam FC 

Dakika ya 36 Sure Boy anapeleka mashambulizi Yanga

Dakika ya 32 Chirwa anapaisha akiwa peke yake karibu na lango la Yanga

Dakika ya 27 Yacouba anasepa na kijiji anafanya jaribio linaokolewa na kipa

Dakika ya 22 Yanga wanapata kona ya kwanza

Dakika ya 21 Tigere anapiga kona ya pili kwa Azam FC 

Dakika ya 19 Sebo anapeleka mashambulizi Yanga

Dakika ya 17 Niyonzima anapeleka mashambulizi Azam FC

Dakika ya 14  Kibwana Shomari anapiga shuti ndani ya 18 linakwenda nje ya lango

Dakika ya 13 Sarpong anaotea

Dakika ya 9 Mukoko anapiga faulo haileti bao

Yanga 0-0 Azam FC


Dakika ya 2 Shikalo anaokoa hatari na Azam wanacheza kona ya kwanza.


Dakika ya kwanza Tigere anafanya jaribio linaokolewa na Farouk Shikalo

4 COMMENTS:

  1. Kocha wa Yanga anapokosea tu ni kumchezesha Sarpong ambae tayari ameonyesha kushindwa, kama nikutegemea umbile na nguvu zake ni kazi bure kwani anautumia mwili wake mkubwa kujiangusha angusha hovyo na kutupa tupa mikono hewani. Sarpong amechangia sana kushuka kiwango kwa Waziri Junior, sababu anakaa benchi sana na anapoteza hali ya kujiamini, huwezi kujiamini kama kocha hakuamini na hakupangi, hata ukiingia kucheza dakika chache utakosa utulivu utaishia kucheza kwa hofu na presha kubwa na kuzidi kukosa magoli. GSM kama mnalazimisha Sarpong apangwe kwakuwa mnamlipa mshahara mkubwa na mmemsajili kwa hela nyingi, muajirini kwenye kiwanda chenu cha magodoro hata awe kuli wakubeba magodoro mpaka mkataba wake utakapoisha. Sarpong sio mwanasoka ni mwana mieleka ndio maana katika mechi anajiangusha sana kuliko kupiga mashuti golini.

    ReplyDelete
  2. Wewe yawezekana umeishavuta kitu cha arusha ndio maana hata unachokiandiki ni upumbavu mtupu

    ReplyDelete
  3. Tatizo letu Watanzania kila mtu ni kocha na ndo maana hatuendi popote

    ReplyDelete
  4. Unamuweka bench mchezaji aliyepokelewa kama mfalme na wakati huo huo ulishajinasibu kuwa ulihusika kwenye usajili, utawaeleza nn utopolo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic